Kwanini Stendi ya makumbusho bidhaa inayotawala ni BISI(Popcon) wakati Gongo la Mboto stand ni NYAMA ZA KUKU wa Kisasa na Matikiti maji?

matunduizi

JF-Expert Member
Aug 20, 2018
6,585
15,366
Wakuu hata kama hainihusu, na sio mteja ila nimepita hizi stendi mara kadhaa hasa mida ya jioni nimegundua hayo.
najiuliza sababu ni nini?

Kumbe wapanda daladala nao wana matabaka ya ununuzi wa bidhaa au ni mkakati wa wamiliki wa hizo stand?

Chanzo na sababu nini? pamoja na ukwere wangu wote hili nimetoka kapa aisee.
 
Na kww nini stand ya mwenge ilikuwa imetawaliwa na nguo za kike za mitumba? Kwa nini makumbusho imetawaliwa na biashara ya viatu, kwa nini stand ya bugurun chama imetawaliwa na nyama za kuku, mbuzi na macangudoa?
 
wakuu hata kama hainihusu, na sio mteja ila nimepita hizi stendi mara kadhaa hasa mida ya jioni nimegundua hayo.
najiuliza sababu ni nini?
kumbe wapanda daladala nao wanamatabaka ya ununuzi wa bidhaa au ni mkakati wa wamiliki wa hizo stand?

chanzo na sababu nini? pamoja na ukwere wangu wote hili nimetoka kapa aisee.
Kwanini baa za banana zimetawaliwa na kitimoto kuliko vyakula vingine?
 
Ni ile tabia ya uswahili tu wachuuzi wanaigana. Hakuna jipya alafu vyakula vya mavituoni mi sifagilii kabisa. Ulichoandika kina uhalisia. Nimepita kote huko.
 
Ni
wakuu hata kama hainihusu, na sio mteja ila nimepita hizi stendi mara kadhaa hasa mida ya jioni nimegundua hayo.
najiuliza sababu ni nini?
kumbe wapanda daladala nao wanamatabaka ya ununuzi wa bidhaa au ni mkakati wa wamiliki wa hizo stand?

chanzo na sababu nini? pamoja na ukwere wangu wote hili nimetoka kapa aisee.
ukweli mtupu, mawasiliano, nguo, ila wamejitahidi kuzuia kwa mule ndani kutokufanya biashara.
 
Goms wengi wanashuka kuelekea majumbani ndo mana vitoweu vinaliwa tofauti na akumbusho.
 
Goms wengi wanashuka kuelekea majumbani ndo mana vitoweu vinaliwa tofauti na akumbusho.
mkuu hii sababubya gomzi inaukweli mwingi sana, kuna dada mmoja anasema yeye akishuka anabeba kipapatio, au kidali akifika nyumbani ni ugali kuku analala.
wazee wa vichwa, utumbo na miguu nao huwa wapo pale kila mtu anakula kulingana na kipato, siku zinaenda.
 
Buguruni Rozana mishkaki
Ubungo mikate imetawala aisee
Posta magazeti tu
Mbagala kwetu kandoro tu

haya maisha hayako fair kabisa
mbezi kwenye zile ngazi za kushuka pale huwa kuna population ya kufa mtu.
pale kila kitu ni vurugu kubwa, labda Tanroad wakiwepo huwa wanatimuliwa hasa usiku.

ni mwendo wa kupambana na hali hadi kieleweke.
 
Back
Top Bottom