Mbona watu wanataka kuwasafisha kina Sitta na wakati alikuwa na yeye anatuhuma kibao za ufisadi? Nadhani kwa ujumla hakuna msafi CCM. Wote wamekaa na kula pamoja. Ni kama sisi tuibe wote, alafu wewe uchomoke na kuanza kusema mimi ndo mwizi. Hali halisi ni kwamba, wote ni fisadi. Na kwa namna moja au nyingine wamehusika katika utumizi mbovu wa pesa za umma. Siku izi fisadi wamepewa title ya WAPIGANAJI. Hizi ni spins tu. Kama wewe ni fisadi, utabaki fisadi.