Kwanini Rose Kamili si kamili

Kwanini Rose Kamili si kamili

singidadodoma

JF-Expert Member
Joined
Nov 11, 2013
Posts
4,394
Reaction score
1,538
MALUMBANO ya kisiasa nchini yanazidi kupamba moto baada ya mke wake wa zamani wa Katibu Mkuu wa zamani wa Chadema Dk Willibrod Slaa, Rose Kamili kuibuka na kusema amesikitishwa na kauli alizozitoa mume wake huyo alipozungumza na waandishi wa habari Septemba Mosi.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Kamili alisema wakati Dk. Slaa anatangaza kung’atuka kwenye siasa alisema amekuwa akila mihogo na familia yake, jambo ambalo si la kweli. Alisisitiza kuwa japokuwa mihogo siyo chakula kibaya, lakini watoto wake, Elimiana na Linus Slaa hawakuwahi kuishi kwa kutegemea chakula hicho ingawa walitelekezwa na baba yao tangu mwaka 2010.

Kamili ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu wa Chadema, alisema Dk Slaa aliwadanganya wananchi aliposema kuwa haongei na mgombea wa urais wa Chadema anayeungwa mkono na Ukawa, Edward Lowassa na Waziri Mkuu wa zamani Frederick Sumaye kuwa siyo kweli kwa kuwa amekuwa akiwasiliana na viongozi hao.

Alisimulia kuwa mwaka 1995 wakati Dk Slaa alipoenguliwa na CCM kugombea ubunge Jimbo la Karatu, alikwenda nyumbani kwa Lowassa kuomba ushauri. Lowassa alimshauri ajiunge na chama chochote na kuongeza kwamba marafiki zake Dk Slaa nao walimshauri aingie chama chochote.

Alisema anamshangaa anavyosema haongei na Lowassa na kuhoji hizo chuki anazosema yeye kama padri mstaafu zinatoka wapi? Kwa hakika, Mama Kamili ameshindwa kuonyesha uongo wa Dk Slaa zaidi ya kuidhalilisha familia yake.

Nasema hivyo kwa sababu kauli ya Dk Slaa kuwa alikuwa akishindia mihogo na familia yake ili aisadie Chadema ni lugha ya picha ambayo haikuwa na maana kuwa kweli walikuwa wakila mihogo.
Alichokuwa akimaanisha Dk Slaa ni jinsi alivyojitolewa kuisaidia Chadema kwa hali na mali ikiwamo kutokuwa karibu na familia yake na hata wakati mwingine kulazimika kutoa fedha zake yake ya mfukoni ili chama hicho kiimarike, lakini hakumanisha familia ilikuwa ikilala njaa.

Sidhani kama Mbunge huyo hajui lugha za alama kiasi kwamba alazimishe kupindisha maneno ya mzazi mwezake kwa ajili ya kunufaisha Ukawa. Kama Mama Kamili anadiriki kumsema Dk Slaa kuwa anatumiwa kisiasa na CCM kwa kuwa alisema aliyoyasema, anataka kutuambia hata yeye basi anatumiwa na Ukawa kumdhalilisha mzazi mwenzake hadharani?

Ni jambo la hatari sana mama huyu kukubali kuisambaratisha familia yake kwa kukubali kutumika kisiasa kisiasi hicho. Tuhuma kwamba Dk Slaa ni dhaifu kwa wanawake tena likitolewa mbele ya watoto wake, linaonyesha kuwa Rose Kamili hajakamilika.

Nasema hajakamilika kwa sababu kwa mwanamke ambaye amekamilika huwezi kuwabeba watoto wako wakubwa wenye watoto wao kwenda kumdhalilisha mzazi mwezako katika televisheni. Hii kwanza inawajengea watoto chuki dhidi ya baba yao na kingine kuwadhalilisha mbele ya jamii.

Kama Rose Kamaili anadai kuwa ametelekezwa na Dk. Slaa tangu mwaka 2010, alipeleka wapi mashtaka ya kutelekezwa ? Je, anataka kuuaminisha umma kwamba Dk Slaa hajali familia yake?
Naamini Rose Kamili ni Mbunge ambaye anajua haki zake kwa vyovyote vile hangeweza kwa muda wote ule kukaa kimya wakati anaonewa, hadi leo ndipo aibuke. Rose Kamili anacheza siasa, tena siasa zenyenye ni nyepesi ambazo hazina mashiko.

Tuhuma nyingine kwamba Dk Slaa kaahidiwa ubunge na uwaziri kama CCM itashinda. Nayo ni hoja nyepesi kwa sababu hivi kiongozi akikosoa Chadema lazima awe anatumika ?
Ina maana Chadema inaongozwa na malaika ambayo haina matatizo kiasi kwamba ionekane kwamba mtu akiinyoshea kidole kuikosoa tayari huyo anatumika na CCM ?

Nadhani Rose Kamili na watu wengine wenye mwelekeo kama huo wanapaswa kufahamu kwamba kila mahali kuna mazuri na mabaya. Alichokifanya Padri Dk Slaa kuonyesha hisia zake za kutofautiana na mawazo ya wenzake kuhusu ujio wa mgombea wa urais kupitia Katibu ya Wananchi (Ukawa), Edward Lowassa.

Ndiyo maana baada ya kuona kuwa mawazo yake yamezidiwa na wengine wakati akiona kuwa kushiriki katika jambo hilo ni kuumiza nafasi yake aliamua kuandika barua ya kujiuzulu wadhifa wa katibu mkuu wa Chadema.

Hiyo ndiyo demokrasia ya kweli kwenye jambo ambalo unaona hukubaliani nalo. Uamuzi wa Dk Slaa sio wa kwanza kufanyika unafanyika katika vyama vingine.

Uamuzi alioufikia aliyekuwa Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba wa kujiuzulu wadhifa wake kupinga kukaribishwa kwa Lowassa ndani ya Ukawa, unafanana sana na ule wa Dk Slaa.

Huwezi kusema kuwa viongozi hao wote kwa umoja wao wamehongwa na CCM ili kuihujumu Ukawa. Mbona hivi sasa tunashuhudia makada wengi wa CCM wanahamia Ukawa, ina maana nao wamehongwa ?
Mhemuko wa kisiasa uliopo sasa nchini usiwe kikwazo, watu waachwe atoe uamuzi wao wa kuhamia chama kipi ili mradi hawavunji sheria za nchi.

Chanzo Raia Tanzania
 
Dr. Slaa sio mwanaume wa kwanza kuachana na mwanamke msumbufu, na hii imedhihirishwa na yanayofanywa na Rose Kamili! Na kizuri zaidi ni kwamba Dr. Slaa kamuacha mama huyo pazuri sana!
HIVI MUNGU AMPE NINI ROSE KAMILI?
 
Hamna rangi mtaacha ona mwaka huu nyie maccm
 
..nyie si mlishaambiwa tatizo ni 'u-first lady', hizi ngonjera nyingine mnazitoa wapi? tatizo lipo chumbani kwa huyo dr wenu,acheni kuhangaika na waliopo mbali..
 
Kuachana na mwanamke uliyekuzalia watoto si jambo zuri lkn kwa mwanamke kama rose kamili bora kuwa kutokuwa na mwanamke ukaishi kapera kulikokuwa na huyu mama. Dk alivumulia mengi sana kwa huyu mama
 
Hamna rangi mtaacha ona mwaka huu nyie maccm
Nimeukumbuka sana huu wimbo leo. "Wanawake wazuri wazuri wameolewa yamebaki manungayembe yanahangaika" mtunzi wake sijui alifikiri nini?
 
Kamili ni jina kama majina mengine na wala sio ukamilifu wa mtu, pia jina hilo ni la pili kwake.
 
Dr. Slaa sio mwanaume wa kwanza kuachana na mwanamke msumbufu, na hii imedhihirishwa na yanayofanywa na Rose Kamili! Na kizuri zaidi ni kwamba Dr. Slaa kamuacha mama huyo pazuri sana!
HIVI MUNGU AMPE NINI ROSE KAMILI?
ila slaa pia sio mwanaume anayejua wanawake wanataka nini

He is a true loser na package aliyofaidika nayo kubwa sana

Mushumbusi ni shiiiiiida kuliko wife #1

Hivi mmeona uke mkologu wa mushumbuzi?
 
Kamili ni kamili kakumbatia vifaranga vyake mpaka vikakua wakati baba yuko kwa kimada akira uroda kwa mgoni wa mahimbo
 
Mama hakusoma language bahati mbaya nikikutana naye ntamfundisha topic ya semantics bure ili imsaidie kumlindia ka heshima kake feki alikonako, hajuhi nini maana ya lugha kitu ambacho hata mwanafunzi wa literature fomu two anaweza kuelewa vizuri kitu kinaitwa literary meaning. Huyu mama ana tatizo la kisaikolojia kwasababu anaongea sana akijiegemeza sana katika hisia badala ya uharisia, atwambie toka 2010 kwanini hajawahi kwenda ustawi wa jamii ama mahakamani kudai fidia? atwambie wanawake wanaotelekezwa huwa wanaitisha press na kuongea ya familia zao ama sheria inawataka wafanyeje, je, press aliyoita ndo itampatia haki yake sasa kama ipo kweli? alafu mbona kama hana akiri vile, kwani watu kiasi gani wanaachana, sasa iweje yeye ndo ajione exceptional mpaka akatangaze, kwani kuachwa kaanza yeye? alafu anafundisha nini kwa wenzie, kwamba watu wakiachana wakaitishe press? alafu anatafutaje huruma yetu wakati hayo ni mambo ya kifamilia, kwani wakati wanaoana sisi tulikuwepo?. Kwa hili na mie nampongeza Dr.Slaa kuachana na huyu mama asiye na haya, mwanamke wa hivi hata kwa bure ni vigumu kumchukua, sijuhi ni malezi, tabia ama ndo taratibu za huko atokako ..basi tu.
 
Khaa!! Mama Kamili kakurupuka. Hata kula mihogo hajui maana yake?? Anawaza kwamba kuna sahani ya mihogo mezani. Mzee Mkapa alikuwa sahihi sana :glasses-nerdy:
 
Kuachana na mwanamke uliyekuzalia watoto si jambo zuri lkn kwa mwanamke kama rose kamili bora kuwa kutokuwa na mwanamke ukaishi kapera kulikokuwa na huyu mama. Dk alivumulia mengi sana kwa huyu mama

mengi kama yapi alikuwa anayavumilia,uwe wazi walau kdg,inaonekana ulikuwa karibu sana na rose kumsaidia mmewe.
 
duh! Mtapindisha maneno hadi mate yawakauke,slaa kasema mwenyewe kuwa walikuwa wana kula mihogo,wewe unapindisha.ina maana slaa hajui hy lugha unayotaka kutuaminisha?au ww ndo msomi zaidi yake,haya tutafsirie na jinsi alivyorushiwa mabegi nje kwa sbb ww ni mtaalamu zaidi,au alikuwa anasafiri ucku huo,ndo mana nampendaga masaburi.
 
Kuachana na mwanamke uliyekuzalia watoto si jambo zuri lkn kwa mwanamke kama rose kamili bora kuwa kutokuwa na mwanamke ukaishi kapera kulikokuwa na huyu mama. Dk alivumulia mengi sana kwa huyu mama

mengi kama yapi alikuwa anayavumilia,uwe wazi walau kdg,inaonekana ulikuwa karibu sana na rose kumsaidia mmewe.
 
MALUMBANO ya kisiasa nchini yanazidi kupamba moto baada ya mke wake wa zamani wa Katibu Mkuu wa zamani wa Chadema Dk Willibrod Slaa, Rose Kamili kuibuka na kusema amesikitishwa na kauli alizozitoa mume wake huyo alipozungumza na waandishi wa habari Septemba Mosi.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Kamili alisema wakati Dk. Slaa anatangaza kung’atuka kwenye siasa alisema amekuwa akila mihogo na familia yake, jambo ambalo si la kweli. Alisisitiza kuwa japokuwa mihogo siyo chakula kibaya, lakini watoto wake, Elimiana na Linus Slaa hawakuwahi kuishi kwa kutegemea chakula hicho ingawa walitelekezwa na baba yao tangu mwaka 2010.

Kamili ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu wa Chadema, alisema Dk Slaa aliwadanganya wananchi aliposema kuwa haongei na mgombea wa urais wa Chadema anayeungwa mkono na Ukawa, Edward Lowassa na Waziri Mkuu wa zamani Frederick Sumaye kuwa siyo kweli kwa kuwa amekuwa akiwasiliana na viongozi hao.

Alisimulia kuwa mwaka 1995 wakati Dk Slaa alipoenguliwa na CCM kugombea ubunge Jimbo la Karatu, alikwenda nyumbani kwa Lowassa kuomba ushauri. Lowassa alimshauri ajiunge na chama chochote na kuongeza kwamba marafiki zake Dk Slaa nao walimshauri aingie chama chochote.

Alisema anamshangaa anavyosema haongei na Lowassa na kuhoji hizo chuki anazosema yeye kama padri mstaafu zinatoka wapi? Kwa hakika, Mama Kamili ameshindwa kuonyesha uongo wa Dk Slaa zaidi ya kuidhalilisha familia yake.

Nasema hivyo kwa sababu kauli ya Dk Slaa kuwa alikuwa akishindia mihogo na familia yake ili aisadie Chadema ni lugha ya picha ambayo haikuwa na maana kuwa kweli walikuwa wakila mihogo.
Alichokuwa akimaanisha Dk Slaa ni jinsi alivyojitolewa kuisaidia Chadema kwa hali na mali ikiwamo kutokuwa karibu na familia yake na hata wakati mwingine kulazimika kutoa fedha zake yake ya mfukoni ili chama hicho kiimarike, lakini hakumanisha familia ilikuwa ikilala njaa.

Sidhani kama Mbunge huyo hajui lugha za alama kiasi kwamba alazimishe kupindisha maneno ya mzazi mwezake kwa ajili ya kunufaisha Ukawa. Kama Mama Kamili anadiriki kumsema Dk Slaa kuwa anatumiwa kisiasa na CCM kwa kuwa alisema aliyoyasema, anataka kutuambia hata yeye basi anatumiwa na Ukawa kumdhalilisha mzazi mwenzake hadharani?

Ni jambo la hatari sana mama huyu kukubali kuisambaratisha familia yake kwa kukubali kutumika kisiasa kisiasi hicho. Tuhuma kwamba Dk Slaa ni dhaifu kwa wanawake tena likitolewa mbele ya watoto wake, linaonyesha kuwa Rose Kamili hajakamilika.

Nasema hajakamilika kwa sababu kwa mwanamke ambaye amekamilika huwezi kuwabeba watoto wako wakubwa wenye watoto wao kwenda kumdhalilisha mzazi mwezako katika televisheni. Hii kwanza inawajengea watoto chuki dhidi ya baba yao na kingine kuwadhalilisha mbele ya jamii.

Kama Rose Kamaili anadai kuwa ametelekezwa na Dk. Slaa tangu mwaka 2010, alipeleka wapi mashtaka ya kutelekezwa ? Je, anataka kuuaminisha umma kwamba Dk Slaa hajali familia yake?
Naamini Rose Kamili ni Mbunge ambaye anajua haki zake kwa vyovyote vile hangeweza kwa muda wote ule kukaa kimya wakati anaonewa, hadi leo ndipo aibuke. Rose Kamili anacheza siasa, tena siasa zenyenye ni nyepesi ambazo hazina mashiko.

Tuhuma nyingine kwamba Dk Slaa kaahidiwa ubunge na uwaziri kama CCM itashinda. Nayo ni hoja nyepesi kwa sababu hivi kiongozi akikosoa Chadema lazima awe anatumika ?
Ina maana Chadema inaongozwa na malaika ambayo haina matatizo kiasi kwamba ionekane kwamba mtu akiinyoshea kidole kuikosoa tayari huyo anatumika na CCM ?

Nadhani Rose Kamili na watu wengine wenye mwelekeo kama huo wanapaswa kufahamu kwamba kila mahali kuna mazuri na mabaya. Alichokifanya Padri Dk Slaa kuonyesha hisia zake za kutofautiana na mawazo ya wenzake kuhusu ujio wa mgombea wa urais kupitia Katibu ya Wananchi (Ukawa), Edward Lowassa.

Ndiyo maana baada ya kuona kuwa mawazo yake yamezidiwa na wengine wakati akiona kuwa kushiriki katika jambo hilo ni kuumiza nafasi yake aliamua kuandika barua ya kujiuzulu wadhifa wa katibu mkuu wa Chadema.

Hiyo ndiyo demokrasia ya kweli kwenye jambo ambalo unaona hukubaliani nalo. Uamuzi wa Dk Slaa sio wa kwanza kufanyika unafanyika katika vyama vingine.

Uamuzi alioufikia aliyekuwa Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba wa kujiuzulu wadhifa wake kupinga kukaribishwa kwa Lowassa ndani ya Ukawa, unafanana sana na ule wa Dk Slaa.

Huwezi kusema kuwa viongozi hao wote kwa umoja wao wamehongwa na CCM ili kuihujumu Ukawa. Mbona hivi sasa tunashuhudia makada wengi wa CCM wanahamia Ukawa, ina maana nao wamehongwa ?
Mhemuko wa kisiasa uliopo sasa nchini usiwe kikwazo, watu waachwe atoe uamuzi wao wa kuhamia chama kipi ili mradi hawavunji sheria za nchi.

Chanzo Raia Tanzania

unasema kaamua kuisambaratisha familia?.
fikiri vizuri juu ya hili.
nini maana ya familia.
na je mpaka hyu mama anasema hivo hii ilikuwa ni familia iliyo pamoja ama ilosambaratika?.
sitaki kukuuliza nani kaisambaratisha.
unaposema lugha ya picha unataka kutufundisha kuwa kila anachoongea slaa huwa si cha kweli maana vingine kumbe huwa anaongea kukoleza tu.sasa mtu anaejiita mkweli iweje awe na maneno ya kukoleza hisia ili kuongeza uzito wa anachoongea?.hii ni tabia ya kike na ya wapenda uongo na hadaa.kwa kariba yake slaa alipaswa nyeusi aite nyeusi na nyeupe aite nyeupe maana baada ya slaa kuondoka cdm mmeanza kumuita mkweli wakati awali mlimwita muongo.
 
MALUMBANO ya kisiasa nchini yanazidi kupamba moto baada ya mke wake wa zamani wa Katibu Mkuu wa zamani wa Chadema Dk Willibrod Slaa, Rose Kamili kuibuka na kusema amesikitishwa na kauli alizozitoa mume wake huyo alipozungumza na waandishi wa habari Septemba Mosi.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Kamili alisema wakati Dk. Slaa anatangaza kung’atuka kwenye siasa alisema amekuwa akila mihogo na familia yake, jambo ambalo si la kweli. Alisisitiza kuwa japokuwa mihogo siyo chakula kibaya, lakini watoto wake, Elimiana na Linus Slaa hawakuwahi kuishi kwa kutegemea chakula hicho ingawa walitelekezwa na baba yao tangu mwaka 2010.

Kamili ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu wa Chadema, alisema Dk Slaa aliwadanganya wananchi aliposema kuwa haongei na mgombea wa urais wa Chadema anayeungwa mkono na Ukawa, Edward Lowassa na Waziri Mkuu wa zamani Frederick Sumaye kuwa siyo kweli kwa kuwa amekuwa akiwasiliana na viongozi hao.

Alisimulia kuwa mwaka 1995 wakati Dk Slaa alipoenguliwa na CCM kugombea ubunge Jimbo la Karatu, alikwenda nyumbani kwa Lowassa kuomba ushauri. Lowassa alimshauri ajiunge na chama chochote na kuongeza kwamba marafiki zake Dk Slaa nao walimshauri aingie chama chochote.

Alisema anamshangaa anavyosema haongei na Lowassa na kuhoji hizo chuki anazosema yeye kama padri mstaafu zinatoka wapi? Kwa hakika, Mama Kamili ameshindwa kuonyesha uongo wa Dk Slaa zaidi ya kuidhalilisha familia yake.

Nasema hivyo kwa sababu kauli ya Dk Slaa kuwa alikuwa akishindia mihogo na familia yake ili aisadie Chadema ni lugha ya picha ambayo haikuwa na maana kuwa kweli walikuwa wakila mihogo.
Alichokuwa akimaanisha Dk Slaa ni jinsi alivyojitolewa kuisaidia Chadema kwa hali na mali ikiwamo kutokuwa karibu na familia yake na hata wakati mwingine kulazimika kutoa fedha zake yake ya mfukoni ili chama hicho kiimarike, lakini hakumanisha familia ilikuwa ikilala njaa.

Sidhani kama Mbunge huyo hajui lugha za alama kiasi kwamba alazimishe kupindisha maneno ya mzazi mwezake kwa ajili ya kunufaisha Ukawa. Kama Mama Kamili anadiriki kumsema Dk Slaa kuwa anatumiwa kisiasa na CCM kwa kuwa alisema aliyoyasema, anataka kutuambia hata yeye basi anatumiwa na Ukawa kumdhalilisha mzazi mwenzake hadharani?

Ni jambo la hatari sana mama huyu kukubali kuisambaratisha familia yake kwa kukubali kutumika kisiasa kisiasi hicho. Tuhuma kwamba Dk Slaa ni dhaifu kwa wanawake tena likitolewa mbele ya watoto wake, linaonyesha kuwa Rose Kamili hajakamilika.

Nasema hajakamilika kwa sababu kwa mwanamke ambaye amekamilika huwezi kuwabeba watoto wako wakubwa wenye watoto wao kwenda kumdhalilisha mzazi mwezako katika televisheni. Hii kwanza inawajengea watoto chuki dhidi ya baba yao na kingine kuwadhalilisha mbele ya jamii.

Kama Rose Kamaili anadai kuwa ametelekezwa na Dk. Slaa tangu mwaka 2010, alipeleka wapi mashtaka ya kutelekezwa ? Je, anataka kuuaminisha umma kwamba Dk Slaa hajali familia yake?
Naamini Rose Kamili ni Mbunge ambaye anajua haki zake kwa vyovyote vile hangeweza kwa muda wote ule kukaa kimya wakati anaonewa, hadi leo ndipo aibuke. Rose Kamili anacheza siasa, tena siasa zenyenye ni nyepesi ambazo hazina mashiko.

Tuhuma nyingine kwamba Dk Slaa kaahidiwa ubunge na uwaziri kama CCM itashinda. Nayo ni hoja nyepesi kwa sababu hivi kiongozi akikosoa Chadema lazima awe anatumika ?
Ina maana Chadema inaongozwa na malaika ambayo haina matatizo kiasi kwamba ionekane kwamba mtu akiinyoshea kidole kuikosoa tayari huyo anatumika na CCM ?

Nadhani Rose Kamili na watu wengine wenye mwelekeo kama huo wanapaswa kufahamu kwamba kila mahali kuna mazuri na mabaya. Alichokifanya Padri Dk Slaa kuonyesha hisia zake za kutofautiana na mawazo ya wenzake kuhusu ujio wa mgombea wa urais kupitia Katibu ya Wananchi (Ukawa), Edward Lowassa.

Ndiyo maana baada ya kuona kuwa mawazo yake yamezidiwa na wengine wakati akiona kuwa kushiriki katika jambo hilo ni kuumiza nafasi yake aliamua kuandika barua ya kujiuzulu wadhifa wa katibu mkuu wa Chadema.

Hiyo ndiyo demokrasia ya kweli kwenye jambo ambalo unaona hukubaliani nalo. Uamuzi wa Dk Slaa sio wa kwanza kufanyika unafanyika katika vyama vingine.

Uamuzi alioufikia aliyekuwa Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba wa kujiuzulu wadhifa wake kupinga kukaribishwa kwa Lowassa ndani ya Ukawa, unafanana sana na ule wa Dk Slaa.

Huwezi kusema kuwa viongozi hao wote kwa umoja wao wamehongwa na CCM ili kuihujumu Ukawa. Mbona hivi sasa tunashuhudia makada wengi wa CCM wanahamia Ukawa, ina maana nao wamehongwa ?
Mhemuko wa kisiasa uliopo sasa nchini usiwe kikwazo, watu waachwe atoe uamuzi wao wa kuhamia chama kipi ili mradi hawavunji sheria za nchi.

Chanzo Raia Tanzania

Kutokuwa kamili kwa huyu mama ni nini? Kwani aliyasema haya Slaa akiwa nyumbani? Je, ni sawa kwa mtu kuitelekeza familia kwa sababu ya hawara? Je, Slaa hakusema anakula mihogo ja maharage? Ni kwanini mnataka aichambue tofauti? Kwa nini hamtaki huyu mama aje na direct meaning ya alichokisema? Ushabiki wa kisiasa unakufanya ushindwe kutumia ubongo wako na tena unakukosesha huruma.
 
Back
Top Bottom