Kwanini Pi Coin Haijalistiwa na Binance

Kwanini Pi Coin Haijalistiwa na Binance

FestoKaguo

Senior Member
Joined
Apr 1, 2022
Posts
128
Reaction score
202
Kwema watu wa JF
Nimeona mtaani watu wakiwa na maswali mengi juu ya kwanini Pi Coin haipo na haijalistiwa kwenye exchange ya Binance au masoko makubwa ya cryptocurrency kama Coinbase, Kraken, na KuCoin. Watu wengi wana matumaini makubwa juu ya Pi Network, lakini bado kuna changamoto kadhaa zinazokwamisha hii ishu. Hapa kwenye hii thread tunaenda kuchambua sababu kuu zinazoifanya Pi Coin kushindwa kulistiwa kwenye exchange ya Binance.

Point ya 1 ni kwamba Mainnet ya Pi network haijakamilika Kamilifu

Taarifa kutoka Pi Network zinaonesha bado Pi hawajafungua Open Mainnet kwa kila mtu. Kwa sasa, mtandao uko kwenye Enclosed Mainnet, ambapo miamala inaweza kufanyika tu kati ya watumiaji waliothibitishwa (KYC) ndani ya mfumo wa Pi Network. Bila blockchain kuwa wazi na kuruhusu miamala kwenye CEX (Centralized Exchanges), haiwezekani kwa Binance kulist Pi.

Point namba mbili ni kwamba Pi network wamekosa uwazi kuhusu teknolojia yao
Exchange kama Binance na masoko mengine makubwa huwa na viwango vya juu vya audition au ukaguzi wa kiufundi kabla ya kuorodhesha tokeni husika. Hadi sasa, Pi Network haijatoa whitepaper ya kina inayoelezea wazi vigezo vya blockchain yake, jinsi mining inavyofanya kazi, na mgawanyo wake wa sarafu kwa undani. Bila hizi taarifa, Binance imeona Pi Coin kama mradi usio na uhakika kwenye teknolojia.

Pia Pi network wameonekana kuwa na Changamoto za KYC (Know Your Customer)
Mojawapo ya kikwazo kikubwa kwa miners wa Pi ni mfumo wa KYC waliouweka ambao umekuwa ukihusisha kuchelewa kwa uthibitishaji wa akaunti. Binance haiwezi kuorodhesha sarafu yenye watumiaji wengi ambao bado hawajathibitishwa. Ili sarafu iwe na thamani kwenye soko, inapaswa kuwa na msingi thabiti wa watumiaji wanaoweza kufanya miamala huru.

Point nyingine ni kwamba Udhibiti na Sheria kwenye Pi network ni hafifu
Mpaka sasa soko la crypto linazidi kudhibitiwa na mamlaka za kifedha duniani. Binance inahakikisha kuwa sarafu zote zinazoingia kwenye soko lake zinakidhi vigezo vya kisheria na uwazi. Mpaka sasa, Pi Network haijatoa taarifa rasmi kuhusu jinsi inavyoshughulikia masuala ya compliance yaani kuzingatia sheria za kifedha, jambo linaloweza kuwafanya Binance kuwa waangalifu zaidi kabla ya kuorodhesha Pi.

Pi network pia Hawana Public Trading au uuzaji wa hadharani
Pi Coin bado haijaanza kuuzwa kwenye blockchain yoyote inayojulikana (kama Ethereum au Binance Smart Chain). Binance haiwezi kuorodhesha tokeni ambayo haiwezi kuuzwa kwa uwazi au kuhamishwa nje ya mfumo wake wa ndani. Mpaka Pi iweze kutumika kama sarafu huru, Binance haiwezi kuilist kwenye soko lake kwa ajili ya kufanyiwa miamala.
Sasa mtu anaweza akaniuliza swali kuwa
Je, Pi Coin Inaweza Kulistiwa Baadaye?

Jibu ni ndiyo, kuna uwezekano mkubwa. Hili litatokea ikiwa:

1.Mainnet itafunguliwa kwa kila mtu

2.Teknolojia itaweka mambo yake wazi zaidi

3.Watumiaji wengi watathibitisha akaunti zao kwa KYC

4.Pi itaruhusu open trading

5.Regulatory compliance itazingatiwa

Kwa sasa, ni vyema kuendelea kufuatilia maendeleo ya Pi Network na kuona hatua zitakazofuata.

Mwisho kabisa nakaribisha maoni yako ndugu msomaji!
 
Sasa ile coin walipeleka OKX kutupiga sio, mim nimeshakubaliana na hali sio mbaya kikubwa uhai tu
 
Mim nilikuwa Nina mine Blum point nikaishia njian


Vip Blum Kuna dalili za hel?
Mim nilikuwa Nina mine Blum point nikaishia njian


Vip Blum Kuna dalili za hel?
Hao mwezi ujao mwishoni wanalist hiyo coin, hawawezi kulist mapema kabla hawajatimiza mipango ya project yao,
 

Attachments

  • Screenshot_20250330-131026.png
    Screenshot_20250330-131026.png
    628 KB · Views: 25
Mim nilikuwa Nina mine Blum point nikaishia njian


Vip Blum Kuna dalili za hel?
Hapana walifanya unyama fulani hivi ulioingiza mkenge watu wengi sana mkuu waligawa zawadi kwa watu laki moja kati ya milioni 57
 
Mimi huwa nawaambia as long as ni ku-click tu hiyo simu yako, hamna neno. Jaribuni tu huwezi kujua yajayo... ili mradi usiwekeze moyo wako hapo ukidhani una utajiri.
Sahihi lakini shida inakuja kwa watumiaji wenyewe mkuu wengi wao wanaamini kuwa thamani ya Pi ni $314K kitu ambacho hata ukimuelekeza mhusika vipi hakuelewi inabidi ukae kimya tu uachane nae
 
Sasa ile coin walipeleka OKX kutupiga sio, mim nimeshakubaliana na hali sio mbaya kikubwa uhai tu
Kwa uzoefu wangu wa cryptocurrency Pi alivyolistiwa OKX na kama mtu aliyemine alikuwa na uwezo wa kuzihamisha kutoka huko kwenye mainnet kuja OKX ningeshauri aziconvert kuja USDT kisha baadae zilivyoshuka mpaka $0.6 angezinunua tena kisha angekuja kuziuza at $1.8 lakini kama watumiaji wote wa app ya Pi mlishindwa kuzimigrate kuja OKX hapo nina wasi wasi na hiyo project niwe muwazi
 
Kwa uzoefu wangu wa cryptocurrency Pi alivyolistiwa OKX na kama mtu aliyemine alikuwa na uwezo wa kuzihamisha kutoka huko kwenye mainnet kuja OKX ningeshauri aziconvert kuja USDT kisha baadae zilivyoshuka mpaka $0.6 angezinunua tena kisha angekuja kuziuza at $1.8 lakini kama watumiaji wote wa app ya Pi mlishindwa kuzimigrate kuja OKX hapo nina wasi wasi na hiyo project niwe muwazi
Wengi hatuja mine ila tuliinunua baada ya wao kuilist kwenye blockchains.
 
Wengi hatuja mine ila tuliinunua baada ya wao kuilist kwenye blockchains.
Nilikuwa mmoja wa walionunua iliposhuka mpaka $0.6 ila ilivyopanda tena nikauza nikatoa hela zangu nikapeleka Binance nikauza maana coin za KUHODL zinajulikana
 
Nilikuwa mmoja wa walionunua iliposhuka mpaka $0.6 ila ilivyopanda tena nikauza nikatoa hela zangu nikapeleka Binance nikauza maana coin za KUHODL zinajulikana
mim nimepigwa aisee nilinunua kipindi ipo moto 2.6 nikiamini kwa moto ule mpaka mwezi my lazima itakuwa usd 5 matokeo yake ndio hivyo unavyoona mpaka sasa
 
Back
Top Bottom