Yericko Nyerere
JF-Expert Member
- Dec 22, 2010
- 17,005
- 20,423
Kufuatia kashifa inayomkumba mkuu wa mkoa wa Dar Paul Makonda ambaye jina lake halisi ni Daudi Albert Bashite, kuna mambo mengi yanajitokeza na yataendelea kujitokeza. Kuna nadharia inayothibitisha kwa 100% kwamba madai haya yanaukweli kwa kila nukta. Na hata vyanzo jadidi vinathibitisha hili.
Sasa kunaibuka kundi kubwa la watu wajinga na wengine kuwa fuata mkumbo na wachache wenye akili ni wanafiki wa kutupwa. Kipo kikundi kidogo hiki kinaonyesha kimetopea kwenye ujinga na huenda shibe yao inatokana na matumizi sahihi ya ujinga wao mbele ya welevu wachache wanafiki kupindukia. Kikundi hiki kimeibuka na hoja kwamba Makonda ni mchapa kazi hivyo kashfa inayomkumba haimpunguzii sifa ya utumishi kama mkuu wa mkoa, kibaya zaidi kikundi hiki kinainasibisha tuhuma hii na kile kinachoitwa vita dhidi ya madawa ya kulevya ambayo kimsingi Makonda hana mamlaka ya kupambana nayo kwakuiongoza au hata kuisemea tu.
Lakini lipo kundi lingine ni kubwa hili linaimbishwa tu nyimbo vyeti vya Makonda feki, vyeti feki, Makonda kaghushi nk.... Hili kundi ni rahisi tu, ni elimu tu ya dharula inawatosha, hawa nitawapa elimu hapa hapa ada yako ni bando lako tu.
Vyeti vya Paul Christian Makonda ni vyeti HALISI vinavyotambuliwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia baraza la mitihani la Taifa. Hivyo Paul Makonda hana kosa la kughushi vyeti. Hana kosa la kuwa na vyeti feki. Kwa minajiri hiyo, Paul Makonda mkuu wa mkoa wa Dar hatuhumiwi kwakuwa na vyeti feki.
Tuhuma za Paul Makonda ni KUIBA vyeti halali vilivyotolewa na baraza la mitihani ambavyo ni mtu anayeitwa Paul Christian nakutumia kujipatia ajira kwa njia za udanganyifu... Hili ni kosa la jinai. Kisheria Makonda anastahili kufikishwa mahakamani kwa makosa makuu matatu. 1. Kuiba vyeti, 2. Kumdanganya mwajiri (ikulu) na 3.Kujipatia ajira na kulipwa pesa ya umma kinyume na utaratibu.
Kosa la kwanza, baraza la mitihani linatakiwa kumshitaki kwakuiba cheti kisicho chake, kosa la pili anatakiwa kushitakiwa na ikulu kwakumdanganya mwajiri wake (rais), hili ni kosa linaloangukia kwenye sheria ya usalam wa taifa. Makonda hapa amehatarisha usalama wa taifa anatakiwa kufikishwa mahakamani wakuhatarisha usalama wa taifa na maisha ya rais kwa ujumla. Kosa hili laweza kuingizwa kwenye uhaini ambalo adhabu yake ni kifo.
Kosa la tatu ni kujipatia ajira na kulipwa mamilioni ya wa tanzania kinyume na utaratibu, hili ni kosa linaloangukia chini ya sheria ya TAKUKURU,
Makonda ameajiriwa na serikali tangu 2015 kama mkuu wa wilaya akilipwa mshahara unaokadiliwa kuwa ni wa Shilingi 4,800,000 mara miezi 12 = 76,800,000 HASARA.
Mwaka 2016 aliteuliwa kuwa mkuu wa mkoa ambapo mshahara wake unakadiliwa kuwa ni kati ya 6,800,000 mara miezi 16= 108,800,000 HASARA.
108,800,000 + 76,800,000= 185,400,000 JUMLA.
Hiyo ni kodi ya umma imeliwa na mtu asiyestahili, achilia mbali eneo aliloumiza wananchi kwakutenda kinyume na taratibu za nchi. Pesa hiyo ingetumika kujenga madara ya shule zaidi ya kumi na kunusuru uhaba wa madarasa katika shule nyingi jiji Dar es Salaam.
Tunaposema anahitaji kuwajibishwa hatumaanishi kule kutumbuliwa tu,bali kufikishwa mbele ya mahakama ili haki iweze kutendeka zaidi. Katika nchi ambako vyombo vya ulinzi na usalama vipo huru, Makonda kwa sasa alistahili kuwa ameshakamatwa na kufikishwa mahakamani, Kamanda Siro kamishina wa Polisi Dar kiutendaji ndie mwenye dhamana ya kumkamata Makonda bila kusubiri amri toka mahali popote pale kwakuzingatia makosa na sababu nilizoeleza hapo juu, lakini katika hali ya kustaajabisha Makonda ameweza kuondoka nchini kanakwamba hii ni Banana Republic. Waziri wa Utawala Bora Mama Angela Kairuki ndie mwenye dhamana na TAKUKURU, Kwa nadharia hii ya Makonda ilitakiwa TAKUKURU wamkamate bila kusubiri amri toka mahali popote pale ilimradi watimize malengo yao ya kupambana na rushwa za aina hii ya Makonda, lakini leo Makonda anabadilisha vikombe vya kahawa pale Bondeni kanakwamba ametoka Banana Republic.
Bado vyombo hivi havijachelewa na havizuiwi na sheria yoyote, kwakutumia sheria ya polisi wa kimataifa (Interpol) wanaweza kuchukua hatua dhidi ya Makonda hukohuko alipo... Tumeamua kujenga taifa lenye nidhamu na uwajibikaji, nchi haiongozwi kwa mazoe, na hili Rais wetu ameliweka wazi,ni wakati sasa wa watu wa aina ya Makonda washughulikiwe bila kuangalia usoni au historia yao.
Wapo wanaolichukulia kosa la Makonda kama kosa dogo linalostahili kupotezewa ama achwe tu aendelee na kazi, lakini niwaabieni kosa la makonda ni kubwa na nihatari kuliko madawa ya kulevya, ni hatari kubwa kwa mjibu wa sheria ya usalama wa taifa, kuidanganya ikulu ni sawa na jaribio la mauaji kwa rais au uhaini... Huyu ameidanganya ikulu kwa miaka mitatu mfululizo, ikulu yenye macho 365/4, ameaminiwa na rais kwa kiwango kikubwa. Huyu anaingia kwenye sheria ya kuhatarisha usalama wa taifa.
Kama rais akiamua kutumia mamlaka yake kikatiba na kisheria,anaweza kumfukuza nchini yani kumuondolea uraia wake hapa Tanzania kwa kosa hilo.... Ni kosa linalodhoofisha umakini wa ikulu na idara ya usalama wa Taifa, Makonda amedhalilisha mamlaka ya Rais.