Kwanini nimechaguliwa HGE. ?

Huwezi chaguliwa pcb ili hali una D ya physics.
Follow what your heart says.
Anaweza kusoma PCB kabisa mkuu. iko hivi kwa mujibu wa muongozo wa necta(unaweza ukaucheki wwebsite yao) kuchaguliwa form five ikiwa ana C zaidi ya tatu mfano tano... anaingia comb isipokuwa tu asiwe na F kwenye somo lolote la comb, mfano yupo dogo hapa ana D ya Geography lkn kachaguliwa HGE goverment huko kagera. Na wapo wengi tu wana D na wamechaguliwa comb hivyo hivyo. kwahiyo huyu kijana akipambana anaweza endelea na comb yake ya PCB bila shida na hatimaye kutimiza ndoto zake. pia njia ingine aliyoko nayo ni kuchukua Ordinary diploma in Clinical medicine(3yrs) then akifanya kazi miaka miwili mitatu ataweza kuendelea na degree ya Doctor of Medicine!. akimaliza hii diploma ataitwa clinical officer atafanya kazi kama doctor kwenye vituo vya afya,zahanati na baadhi ya hospitali za wilaya na mikoa zenye upungufu wa MD na AMO.
 
Wanaenda certificate mkuu basi tu naona wanachanganya changanya mambo
Diploma ni kwa yule alietoka form six au aliemaliza certificate
Kama amechaguliwa Technical college mfano DIT, ATC, Chuo cha Maji au MUST atasoma kwa miaka mitatu akimaliza atakuwa na Dip au kwa maana nyingine ataanzia
1. Basic Technician Certificate NTA level 4
2. Technician Certificate, NTA level 5
3. Ordinary Diploma, NTA level 6
4. Higher Diploma, NTA level 7

Ambazo hizi level zote ni ndani ya miaka mitatu akimaliza hapo anaweza kusoma Degree( NTA Level 8)
 
Naona ni bora tu nikasomee IT au computer engineering kwasababu ipo moyoni na pia nina ujanja janja wa kurekebisha simu na computer.
Fanya hivyo. Achana na hiyo HGE. Ni vizuri pia kwa kuwa umegundua hiyo "ipo moyoni" kuliko kwenda kusoma kitu kwa kufuata mkumbo.
 
Usiende Advance instead piga Electrical engineering hapa DIT ama ATC Arusha. Ukimaliza utakua na uelewa mpana nini kifuate.

Don give a damn thanking me later. Its facking meaningless
 
Nenda diploma ya eletrical, automobile, civil au mechanical ....huez kosa kazi kama lengo ni ajira...dit, nit, arusha au mbeya tech college.

Thank me later.

Mbeya Technical College??!you can't be serious!!!!!!au unamaanisha MBEYA UNIVERSITY OF SCIENCE AND TECHNOLOGY?!!!
 
Usiende Advance instead piga Electrical engineering hapa DIT ama ATC Arusha. Ukimaliza utakua na uelewa mpana nini kifuate.

Don give a damn thanking me later. Its facking meaningless

👍🏽
 
Huo muongozo wa mwaka gani?.
Ili uchaguliwe tahsusi flani ni lazima uwe na grades kuanzia C au juu ya hapo. Huo ndo muongozo unavyosema huwezi kuwa na ccd ukachaguliwa advance
 
M nakushauri tafta namna ya kubadili kombi ikishindikana tafta coz ya nursing lakn hakikisha unapambana kubadili kombi advance ina raha yake achana na walopitia short cut na wengi unaosikia wanakwambia advance unapoteza mda hawakuchaguliwa kujiunga na hyo advance ndo maana wanalalama tu hapa sitak povu achen kupotoshana
 
mmekutana wote hamjui halafu mnaelekezana njia. mm nilipomaliza f4 nilichaguliwa direct dip pale arusha tech
Uo ulikuwa utaratbu wao ndo maana ukasoma miaka mitatu means waliunga certificate na diploma ila form four leaver anaanza na certificate na sio diploma
 
Hakuna kitu kama hicho! ila vyuo vingi ukianza tu Certificate wanakuita Diploma mwaka wa kwanza urongo mtupu!! Ili wawe na hakika ya ADA yako kwa miaka mitatu
Ndo nilijaribu kumwambia hyo anayedai kaunga diploma hajui wao wanachofanya n two in one
 
Ndivyo ilivyo! hapo first year NTA 4(Certificate), second year NTA 5 (Diploma yr 1) na third year NTA (Diploma yr2) 6!The only thing ni kwamba hufanyi application kwa ajili ya miaka inayofata
ipo hivi NTA 4(basic technician certificate)NTA 5(technician certificate)NTA 6(full technician certificate) ambayo ni ordinary diploma
 
Mkuu, phy na math ndo msingi kama hukupata bahat ni bora ukasome unachotaka maana elimu yetu ya bongo bado kuna shida kweny maswala ya kuchagua watu kulingana matakwa hasa upande wa elimu.
 
Nenda diploma ya eletrical, automobile, civil au mechanical ....huez kosa kazi kama lengo ni ajira...dit, nit, arusha au mbeya tech college.

Thank me later.
Azingatie hilli!
 
Nisaidie hizo hatua mkuu
 
Huo muongozo wa mwaka gani?.
Ili uchaguliwe tahsusi flani ni lazima uwe na grades kuanzia C au juu ya hapo. Huo ndo muongozo unavyosema huwezi kuwa na ccd ukachaguliwa advance
Ndio hivyo ulivyo utaratibu mkuu, ukiwa na d moja kwa kombi unachaguliwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…