Galacha Maestro
JF-Expert Member
- Sep 29, 2011
- 1,353
- 2,220
Unapenda sana mabadiliko kwenye maisha yetu, lakini hakuna viumbe wagumu kubadili kama sisi wenyewe.
Ni rahisi sana kuona wengine ndio wanahitaji kubadilika.
Ni rahisi sana kuongea kuhusu mabadiliko.
Ni rahisi sana kulalamika na kulaumu pale unapoona mambo hayaendi sawa.
Lakini inapofika kwamba unahitaji kubadilika, hapo ndipo ugumu unapoanzia.
KAMA KUNA KITU HUKIPENDI, BADILI.
Wewe ni mwana mafanikio, na ili ufikie mafanikio makubwa zaidi, na uendelee kubaki kwenye kilele cha mafanikio, unahitaji kufanya mabadiliko ya mara kwa mara kwenye maisha yako na kile ambacho unafanya.
Kila inapojisikia kulalamika au kulaumu, acha mara moja na jiulize nibadili nini hapa?
Kwa mfano hutapata kazi au biashara nzuri kwa kulalamikia uliyonayo sasa, ni lazima ubadili kitu.
Hakuna mtu amewahi kuwa na ndoa bora kwa kulalamikia ndoa yake ilivyo mbaya kwa sasa. Ni lazima ukae chini na uone ni vitu gani vya kubadili.
Kitu chochote ambacho ni muhimu sana kwenye maisha yako unaweza kukipata kupitia mpango wa mabadiliko, ambao umejiwekea wewe mwenyewe.
Mpango wa mabadiliko ni mzuri sana kwako, je unao?