Kwanini mwenyekiti wa CCM hajaonyesha mfano wa kujiuzulu uenyekiti na kubaki na kofia moja?

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
48,694
149,920
Kuongoza ni kuonyesha njia hivyo nilitarajia Mwenyekiti wa CCM Taifa, Raisi Magufuli atangaze kujiuzulu na kisha atoe fursa kwa Mkutano Mkuu kumchagua mwenyekiti mwingine ili yeye abaki na kofia moja tu ya uraisi

Sijui utekelezaji wa mabadilko hayo ya 16 ya katiba ya CCM yanaanza lini ila naamini bado ilikuwa ni fursa nzuri kwa mwenyekiti kuonyesha mfano na kutake advantage ya vikao hivyo kufanya uchaguzi mwingine bila kusubiri kuitisha vikao vingine na kuongeza gharama ya kuitisha vikao hivyo vikao ambavyo vingeweza kuepukika(kama kweli alikuwa ana nia hiyo).

Na je, mawaziri kuwa wabunge hii nayo imekaaje?

Wabadili na katiba basi mawaziri wasiwe wabunge ndio tujue wako serious.

Hoja hapa ni kuwa,kwasababu CCM ndio inaunda serikali,kwanini mabadiliko haya yasihusu hata vyeo walivyonavyo ndani ya serikali?
 
Wewe ya CCM yanakuhusu au unaupenda CCM???? Nenda tawi lililopo karibu yako upewe kadi....maana ulivyo na kiherehere cha kufatilia ya wenzako wakati ya kwenu yamewashinda mnatia aibu
 
Wewe ya CCM yanakuhusu au unaupenda CCM???? Nenda tawi lililopo karibu yako upewe kadi....maana ulivyo na kiherehere cha kufatilia ya wenzako wakati ya kwenu yamewashinda mnatia aibu
Unafiki mtupu!Kwenye Bunge la Katiba sio ndio nyie mlipinga mawaziri kutokuwa wabunge?Leo hii busara ya kukataa kofia mbili imetoka wapi?
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Wanafiki tu nyie.Kwenye Bunge la Katiba sio ndio nyie mlipinga mawaziri kutokuwa wabunge?Leo hii busara ya kukataa kofia mbili imetoka wapi?
CCM inaamini kila jambo na wakati wake...kwa kilichofanyika ndani ya CCM leo wakati ulikuwa umefika....hicho unachozu gumza kuhusu katiba ya nchi wakati wake ulikuwa haujafika...ukifika na mahitaji yakawepo suala hilo litafanyika bila hata kusukumana
 
...

Na je, mawaziri kuwa wabunge hii nayo imekaaje?

Wabadili na katiba basi mawaziri wasiwe wabunge ndio tujue wako serious...QUOTE]

Salary Slip: unapoandika humu huwa naamini ni mchambuzi mahili kumbe huleta simulizi za kijiweni zisizo na mshiko, ni tetesi na hoja za umbea tu.

Ebu nikunukulie Ibara ya 55.-(4) ya Katiba ya JMT (1977): Mawaziri na Naibu Mawaziri wote watateuliwa kutoka miongoni mwa Wabunge.

Hivyo si matakwa ya Katiba ya CCM bali ya nchi ambayo wabunge wa vyma vya upinzani walisusia vikao vya Bunge la Katiba na kuunda UKAWA, kumbe nia ikiwa ni CHADEMA kuua vyama vingine!
 
CCM inaamini kila jambo na wakati wake...kwa kilichofanyika ndani ya CCM leo wakati ulikuwa umefika....hicho unachozu gumza kuhusu katiba ya nchi wakati wake ulikuwa haujafika...ukifika na mahitaji yakawepo suala hilo litafanyika bila hata kusukumana
Mahitaji gani yasiyokuwepo sasa ?!
 
CCM inaamini kila jambo na wakati wake...kwa kilichofanyika ndani ya CCM leo wakati ulikuwa umefika....hicho unachozu gumza kuhusu katiba ya nchi wakati wake ulikuwa haujafika...ukifika na mahitaji yakawepo suala hilo litafanyika bila hata kusukumana
Kama uwezo wenu wa kuona mbali ni mdogo bora muwapishe wenye uwezo wa kuona mbali waongoze nchi maana hatuwezi kuwa tunasubiri mpaka nyie muone jambo fulani ni muhimu huku mkiwa mnatuchelewesha.
 
Kama uwezo wenu wa kuona mbali ni mdogo bora muwapishe wenye uwezo wa kuona mbali waongoze nchi maana hatuwezi kuwa tunasubiri mpaka nyie muone jambo fulani ni muhimu huku mkiwa mnatuchelewesha.
Yani CCM ipishe iwaachie nchi akina Wema? Duh nyie mnavichekesho balaa....wewe akili zako fupi ila ujuaji tu ndo mwingi.
 
Yani CCM ipishe iwaachie nchi akina Wema? Duh nyie mnavichekesho balaa....wewe akili zako fupi ila ujuaji tu ndo mwingi.

Mbona huko kwenu ndiyo kuna vichwa mpanzi zaidi ya Wema na bado mnaendesha nchi kwa kudanganywa umma wa Watanzania. Kuna muda utafika uongo wa CCM hautasaidia tena.

Kama mnayoyaita Mabadiliko mmeshindwa kuendesha chama sababu pakuiba hakuna tena kila mahali pamekaza hakuna maposho ya kumwaga.

Hakuna cha kofia moja wala mbili,issue imeshamwagwa hewani mshiko hakuna ndani ya CCM. Wahindi waliokuwa wanawapa pesa wameondoka.

Ndiyo sababu mko busy kunyanyasa raia.
 
Wewe ya CCM yanakuhusu au unaupenda CCM???? Nenda tawi lililopo karibu yako upewe kadi....maana ulivyo na kiherehere cha kufatilia ya wenzako wakati ya kwenu yamewashinda mnatia aibu
Hii ni forum huru kila mtu anaruhusiwa kuleta mada yoyote bila kujali itikadi ili mradi unazingatia sheria kanuni na taratibu za JF
 
Back
Top Bottom