Kwanini Mugabe anatukana Wazungu kwa Kiingereza?

Barbarosa

JF-Expert Member
Apr 16, 2015
22,584
27,817
Hii kitu sijaielewa mpaka leo, Rais Mugabe anawatukana sana Wazungu kwa kifupi anawachukia lkn anayafanya yote haya kwa Kiingereza tena kwenye makao Makuu ya nchi za Kiafrika sasa kwanini asitumie Kishona?
 
Ametengeneza njia gani kwa wazimbabwe?? Kubishana kwake na wazungu kunawasaidia nini wazimbabwe??? Kwa nini angekaa kimya tu akajenga uchumi wa zimbabwe na taifa lake likawa super power nini kingeharibika??? Hajafikia bado level ya kubishana na wazungu, ni North korea pekee ndio wamefikia level ya kubishana na wazungu, huwezi kubishana na wazungu wakati unaimport kila kitu na hauwezi kutengeneza kila kitu hapo utaonekana mwehu tu..
Waafrika bila kujitambua hatutakuja kujua tatizo letu, hatukubali kuteseka kwa manufaa ya kizazi kijacho, hatutumii vichwa vyetu kufikiri na niwepesi wa kutaka kusaidiwa, MUGABE namuona kama wehu wengine ambaye hajui anachokisimamia, haiwezekani ukapambana na wazungu uliowakumbatia na kuwa kibaraka wao miaka nenda rudi halafu pale walipokuambia tu upumzike wengine wawe maraisi shida ndio imeanza,, MUGABE ni mgonjwa wa ile common african disease,, "KUTOKUJITAMBUA" na maslahi binafsi..
 
Hii kitu sijaielewa mpaka leo, Rais Mugabe anawatukana sana Wazungu kwa kifupi anawachukia lkn anayafanya yote haya kwa Kiingereza tena kwenye makao Makuu ya nchi za Kiafrika sasa kwanini asitumie Kishona?
afu ndani ya jengo lililojengwa na haohao wazungu!
 
Hii kitu sijaielewa mpaka leo, Rais Mugabe anawatukana sana Wazungu kwa kifupi anawachukia lkn anayafanya yote haya kwa Kiingereza tena kwenye makao Makuu ya nchi za Kiafrika sasa kwanini asitumie Kishona?
Ili wamuelewe haraka lazima awaambie kwa lugha yao. Kwani we unachukuliaje? We binafsi angetumia kishona ungemuelewa?
 
When you become more older,you think and act like a child.......Ndio Mgabe huyo,tukana huku uwe na uwezo wa kuatatua shida za wananchi wako.Wananchi wanakufa kwa njaa anaiomba dunia imsaidie..akina nani kama sio white faces with big noses!!Huyu mzee hawezi kufukir tena,nafas anayohold sasa does not match with his expired brain.Tusishabikie tu kama mazombie bila kua nafikra pambanuzi.
 
Anataka ujumbe ufike bila chenga, atumie kishona ili mkalimani aogope kusema ukweli ageuze maneno?
 
Ili wamuelewe haraka lazima awaambie kwa lugha yao. Kwani we unachukuliaje? We binafsi angetumia kishona ungemuelewa?

Mbona akina Kim wa Korea, Ahmedinejad wa Iran akina Chaves wanaongea lugha zao na Wazungu wanatafsiri na ujumbe unawafikia?
 
Anataka ujumbe ufike bila chenga, atumie kishona ili mkalimani aogope kusema ukweli ageuze maneno?

Lkn Mzungu ndiyo anazidi kukudharau jaribu tu uwe nafasi ya Mzungu labda tusema mtu ktk Chad au Mali anakuchukia sana anachukia kila kitu chako halafu anatoa hotuba kwa kwa lugha yako huku akiponda kila kitu chako, wewe utajisikiaje? Hautajiuliza mswali, kama mimi ni mbaya hivyo kwake ni kwa nini anatumia lugha yangu? na Je utaendelea kumuheshimu huyu mtu?
 
Back
Top Bottom