Kwanini mtu akikuacha kwa maumivu tena bila hata sababu mara nyingi hupitia magumu na kukukumbuka?

Mr. Sound

JF-Expert Member
Sep 15, 2020
1,166
2,427
Habari wana JF,

Kuna watu hawajui kumuacha mtu kistaarabu, unakuta mtu anakuacha kwa masifa, madharau, nyodo kibao mpaka unadata. Mara nyingi watu wa namna hii mbele yao maishani hupitia misuko suko na kujutia waliyoyafanya hata wakatamani masiku yarudi nyuma ili wasawazishe makosa yao.

Nimewahi kuwa muhanga wa jambo hili kwa binti niliewekeza nikijua ni future wife, daily ananiambia anajutia sana kumuacha mtu mwenye upendo wa kweli, ananiambia licha ya kuwa tayari nina mke nimfikirie tu maana hana amani maishani mwake kwa nyakati ngumu anazopitia, mimi nimemuweka wazi, haiwezekani hata kwa bahati mbaya japo nishamsamehe lakini daily hachoki kunitafuta.
 
The Power of Karma, ukiskia Mungu hushindia watu vita wasivyoviweza ndio kama hivyo yani.

Mtu akiachana na wewe kwa vishindo kwa kuona haufai labda na kujaribu kushusha utu wako ilihali uko innocent basi jua tu ameamua kuku victimize ili atimize lengo lake flani ila huwa kuna namna ya pekee hawa watu hufunzwa na ulimwengu.😂😂😂

Mtu anakumbwa na misuko suko mpaka anaamua kunyoosha mikono juu asijue wapi aliteleza. KARMA!
 
Kuna ex wangu mmoja pisi kali ya maana alikuwa hajali kwenye mahusiano yaani yeye alikuwa akitongozwa kila siku na wanaume. Nikateleza na kuendelea na maisha yangu sasahivi yupo late 20's hadumu na relationship yaani hafiki 4 months kaachwa.


Ndukiiiii 🏃‍♂️🏃‍♂️🏃‍♂️
 
Hata mimi kuna binti anajutia sana kunitenda... Alikokimbilia yanayomkuta ananisimulia mpaka namwambia ni sehemu ya maisha tu ambayo alichagua mwenyewe kua nayo au kuyapitia sabu sikumfukuza!

Kila siku ananitafuta kwa kutaka arudi lakini hata sina muda kabisa japokua sijaoa lakini sina wazo hata chembe la kurudiana nae, Zaidi namtia moyo tu akomae maisha ya ndoa sio lelemama.

Hawa viumbe kuna maisha mengine huwa wanayaona yanawafaa, ukiona hivyo wewe jiweke pembeni tu afu subiri feedbacks kutoka kwa jamaa zake au yeye mwenyewe za huko wanakokimbilia...
 
habari wana jf,

kuna watu hawajui kumuacha mtu kistaarabu, unakuta mtu anakuacha kwa masifa, madharau, nyodo kibao mpaka unadata. mara nyingi watu wa namna hii mbele yao maishani hupitia misuko suko na kujutia waliyoyafanya hata wakatamani masiku yarudi nyuma ili wasawazishe makosa yao.

nimewahi kua mhanga wa jambo hili kwa binti niliewekeza nikujua ni future wife, daily ananiambia anajutia sana kumuacha mtu mwenye upendo wa kweli, ananiambia licha ya kua tayari nina mke nimfikirie tu maana hana amani maishani mwake kwa nyakati ngumu anazopitia, mi nimemweka wazi haiwezekani hata kwa bahati mbaya japo nishamsamehe lakini daily hachoki kunitafuta.
Karma is real.
 
Back
Top Bottom