Kwanini mimi?

Kwanini mimi?

Showio

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2019
Posts
254
Reaction score
482
Kuna siku ,katika maisha yetu kila mtu hutaka majibu halisi ya maswali yanayoibuka kichwani mwake ,kwanini maisha ni magumu ? Kwanini maisha yapo hivi?

Hata tunapolenga shabaha tulizojiwekea sisi wenyewe yaani makusudio au malengo ya maisha yetu tuliojiwekea.Bado tunaendelea kuhisi kama hatuna kitu ,au hatujafanya chochote hadi sasa,ingawa tumeshafanya vitu vingi .Kwanini haturiziki na vitu tulivyonavyo?

Pale tunapokosa kulenga shabaha tulizojiwekea maswali yanayoibuka kichwani yanaweza kuwa mengi zaidi ,kwanini mimi ,Mungu? Kama unanipenda ,una kuwa wapi napo kuhitaji ? kwanini hili linatokea kwangu?

Ikiwa bado hujafanya lolote ambalo ndilo kusudio la wewe kuwa hapa kamwe huwezi kupata utoshelevu,tuendelee kujiuliza na kutafuta majibu ya maswali yanayoibuka vichwani mwetu.
 
Back
Top Bottom