Kwanini mchawi hawezi kuiba hela benki japo anaweza kupenya ndani, kuroga ama kupaa angani

Mdakuzi mkuu

JF-Expert Member
Dec 27, 2016
212
719
Mchawi atafanya mengi.Atakulimisha,atakubeba-beba, atakuchezea weee lakini ujanja wa kuchukua hela benk au nyumbani kwa mtu,wameshindwaa.

Hata kama kuna hela umeziacha sebulen,atazichezea tuu lakin hawezi ondoka nazo.Hata akienda benki, ataogelea kwenye mahela wee,kuyachukua hawezi.

La kujiuliza, ana uwezo wa kuingia ndani au kupaa angani kama ndege,kwann ashindwe kuingia NMB, CRDB, nk kukwapua mapesa yote??
 
Mi naamini uchawi upo lakini uchawi ni kitu DHAIFU SANA kiasi kwamba u aweza tu kumsjmbua sumbua mtu lakini hauwezi kuamua mustakabali (Destiny) ya mtu. Na ukishatambua kwamba uchawi ni dhaifu na kuudharau wala hauwezi kukudhuru kamwe. Wala huhitaji kuwa mlokole ndo uweze kushinda kitu dhaifu kama uchawi
 
Wajinga ndo waliwao, hamna uchawi ni imani tu!
Ukiamini kuna Nuru amini kuna Giza pia
Hata kwenye mafundisho ya dini uchawi unaongelewa.
Kumbuka wakati Yesu anatoka baharini akiwa na wale jamaa wavuvi sijui ndo akina Zakayo sikumbuki majina yao, pale Yesu anakutana na mchawi kwa uwezo wake anamuamuru ondoka zako, kuna nguruwe pale wanatupiwa majini kutoka kwa yule chizi hyo yote ni proof ya nguvu ya Giza ilikuepo tangu enzi

Danger is real but fear is a choice.
Wajuzi wa maandiko watakufafanulia mi siko deep huko
 
ukisoma kwa makini kitabu cha JIFUNZE UCHAWI volume 1 kile kipengele cha tatu a na cha sita b, kimesisitiza kabisa kuwa pesa ni karatasi,pesa huwa pesa nje ya uchawi...ndani ya uchawi hakuna pesa yaani mchawi akiwa uchawini haoni pesa anaona makaratasi. By the way hicho kitabu bado sija ki publish☺
 
Mchawi atafanya mengi.Atakulimisha,atakubeba-beba, atakuchezea weee lakini ujanja wa kuchukua hela benk au nyumbani kwa mtu,wameshindwaa.

Hata kama kuna hela umeziacha sebulen,atazichezea tuu lakin hawezi ondoka nazo.Hata akienda benki, ataogelea kwenye mahela wee,kuyachukua hawezi.

La kujiuliza, ana uwezo wa kuingia ndani au kupaa angani kama ndege,kwann ashindwe kuingia NMB, CRDB, nk kukwapua mapesa yote??
Hii mada ilishajadiliwa sana humu.
 
Bank ni mchawi namba moja ila wachawi wanapopaonea ni izi sehemu za kubadilisha fedha(bureau de change) izo ndio wanzoziibaga
 
Benki wenyewe ni wachawi ni kama migodini hapaingiliki kizembekizembe
 
Back
Top Bottom