Kwanini mahusiano mengi hayawi endelevu?

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,106
10,172
Moja kati ya vitu vinavyowakumba vijana wengi wa kileo, ni kutokuwa na mahusiano endelevu/yanayodumu kwa muda mrefu. Tatizo hili limefanya watu wasifurahie mahusiano yao, au mara nyingine wakiingia katika mahusiano kwa tahadhari kubwa. Bado vijana hawajui wanakosea wapi katika hili, japo ni wao wanaowachagua wapenzi wao tofauti na zamani walikuwa wakichaguliwa. Hapa nipo kutoa darasa kwa vijana ambao wamekuwa waathirika (victims) wakubwa wa hali hii. Na nitataja baadhi ya sababu zinazofanya watu wasifurahie mahusiano yao.

KOSA KUBWA WANALOFANYA VIJANA.

VIJANA WANATAKA HESHIMA KWA KUUZA FURAHA ZAO
Vijana wengi hawapendi kujipa furaha wao, ila kuwafurahisha majirani zao (wenyewe wanasema kuwanyoosha). Hii inafanya vijana wawe na mahusiano na watu ambao watawafanya waheshimiwe, bila kujali watajisikiaje katika mahusiano hayo. Hali hii inatokana na kutokujua kuwa, mahusiano yapo kwa ajili ya furaha ya nafsi na sio heshima kwa marafiki zako.
Vijana wengine wameachana na wapenzi wao kwa sababu marafiki zao huwakandia wakiwaona na wapenzi wao. Hii ni kawaida, kijana anayependa mpenzi wa namna fulani, kumkandia kijana asiyekuwa katika mapenzi yake (preference). Kitu cha kujua ni kwamba kila mtu ana kitu anachokipenda. Mf. Kuna watu wanapenda rangi ya kijani na kuna wengine hupenda rangi nyekundu. Anayependa kijani anaweza kuikandia rangi nyekundu, lakini je ni busara mtu kuacha kupenda nyekundu kisa kuna Rafiki yake haipendi nyekundu? Swala ni kuwa vijana inabidi wajitambue kuwa mapenzi ni mahusiano ya nafsi mbili zinazotafuta kushibana, yapo kwa ajili ya furaha kamili (bliss) na sio kwa ajili ya heshima kwa marafiki, ndugu au jirani zako.

VIJANA HAWAONI UZURI ULIO KWA WAPENZI WAO.
Hapa sasa ndio tatizo hutokea, kwa mfano wa rangi niliotolea hapo juu. Kijana anayependa rangi ya kijani na anajua kwa nini anapenda rangi ya kijani na kuzichukia rangi nyingine anaweza akawa strong katika kutetea mahusiano yake. Lakini kwa kijana anayependa nyekundu bila kujua kwa nini anapenda nyekundu anaweza akawa easily destructed kama atajadili na yule anayejua kwa nini anapenda kijani.
Kwa maana hii ni kwamba wewe uliye na mpenzi lazima ujue kwa nini unampenda mpenzi wako. Kwa nini unampenda mtu mrefu/mweupe/mnene na sio mfupi/mweusi/mwembamba (you may swap). Kama hujui kwa nini unapenda unachokipenda, unaweza ukaanguka katika sababu za mwenzio za kupenda kitu kilicho kinyume na wewe. Hili ni kosa ambalo limefanya vijana waache kupenda wanaowafurahia kwa sababu hawajui kwa nini wapo na wapenzi wao.

UNAIJUA PICHA YA MWENZA UNAYEMTAKA?

Moja kati ya vitu ambavyo Nimekuwa naviamini kwa sasa ni picha ya mtu unayemtaka. Kuna wengine wanajua, wengine hawazijui picha za wanaowahitaji. Kama utakaa na nafsi yako utajua ni ipi picha halisi ya mpenzi unayemtaka. Jiulize hili, ni watu wangapi umekutana nao bila kuwa na mshituko wowote wa hisia za huba? Wangapi ulitamani itokee siku uwaone tena japo ilikuwa ndio kwanza mmekutana? Hapa ndipo nnapoweka concept ya picha, yaani yule unayependa kuwa naye mara kwa mara ndiye anayefanana na picha iliyo kichwani kwako(uwe unajua au hujui). Kama usipojua picha ya unayemuhitaji, unajiweka katika hatari ya kushindwa kumpata yule ambaye nafsi yako itamridhia.

UNAIJUA ”ABSOLUTE BEAUTY”

Moja kati ya kitu kizuri ambacho Plato alikisema kuhusiana na mapenzi ni absolute beauty. Absolute beauty kwa mujibu wa Plato ni ule uzuri ambao unaona wewe unayependa wakati wenzako hawauoni. Inawezekana mpenzi wako ana tabia au Mazoea fulani ambayo watu huona ni mabaya, wewe unaona ndio uzuri wake. Na huu ndio upendo ambao unaleta amani katika nafsi. Kumpenda mtu katika ujinga wake, hekima zake, upumbafu na udhaifu wake. Kama utaona unachofurahia katika upumbavu wa mpenzi wako, haitofika siku ambayo wewe utakereka.

IDEALIZATION

Kutokana na watu kushindwa kuwapenda wapenzi wao vile walivyo, vijana wengi wanawa-idealize wapenzi wao. Mfano mtu hapendi mpenzi wake awe muongeaji, na anashindwa kuona uzuri wa mpenzi wake kuwa muongeaji, anaamua kumu-idealize kwamba ipo siku mpenzi wake atakuwa mkimya. Anaanza kufanya namna mbalimbali za kumfanya mpenzi wake awe mkimya, anajaribu kumtengeneza mpenzi wake vile yeye anataka, na inapotokea mpenzi wake ameshindwa kutengenezeka vile yeye anataka basi ndio huwa mwisho wa mahusiano.
Enyi vijana wapendeni wapenzi wenu jinsi walivyo na sio jinsi unavyodhani anaweza kuwa. Idealization imevunja mahusiano mengi, na mengine hayafurahiwi kabisa.
Katika kurasa hizi niseme hapo vijana tutakuwa tumeelewana, niwape shime ya kumtafuta mtu wa kukupa furaha sio wa kukufanya uheshimiwe na Rafiki zako wakati wewe mwenyewe hufurahii mahusiano hayo. Kila mtu anahitaji amani ya nafsi.

NB: sina muda na mijadala ya ngono. Kama utapenda mijadala na mimi iwe mijadala ya mapenzi.

By Analogia Malenga.
 
Last edited:
Back
Top Bottom