Kwanini mafile ya picha hutofautiana size ?

Ok9

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2013
Posts
4,554
Reaction score
4,171
Kwann ukipiga picha kwa simu...zinatofautiana size ..I mean mb...kb......na unakuta zimepigwa kwa wakati mmoja..?
 
Kwann ukipiga picha kwa simu...zinatofautiana size ..I mean mb...kb......na unakuta zimepigwa kwa wakati mmoja..?

Swali lako ni zuri sana, picha mainly zinakuwa zimetengenezwa na blending colors tatu. Ambazo ni, Red, Green na Blue. Kwa mfano tuchukulie 24 bit za picha kunakuwa kuna 8 bits kwenye kila hizo blending colors.. Na kila zangi kati ya hizo tatu, zinakuwa zinaanzia kipimo cha 0 - 255 .

Zikiwa 0 zote basi picha nzima itakuwa nyeusi. Na zikiwa range ya juu kabisa (ambayo ni 255) basi picha itakuwa nyeupe yote. Hivyo sasa 255 ikiwa kipeo cha tatu itakuwa takribani rangi milioni 16. Kwa hiyo picha ikiwa na details nyingi intensity ya rangi huongezeka. Inapoongezeka ndivyo file size ya picha yako inavyoongezeka.

Kwa hiyo hata kama umepiga picha kwa wakati mmoja, kuongezeka na kupungua kwa details kunasababisha compression ya picha kupungua ama kuongezeka kwa photo file size yako. Natumaini nimekujibu kama ulivyouliza.
 
Nimekukubali mkuu... Ni darasa zuri sana kwa tulio wengi..
 

kuongezea hapa pia kuna resolution ya picha. kwenye simu hapa inaathiriwa na mambo mawili

1.megapixel za camera
2.setting za camera

-jinsi camera ilivyo na megapixel kubwa ndio jinsi picha inavyokuwa kubwa ki mb, kwa sababu resolution ya picha nayo inakuwa kubwa

-setting za camera pia zinasababisha mb zitofautiane. mfano iphone 5 ina 8mp lakini unaweza piga picha za 2mp, inamaana watu wawili wana iphone 5 mmoja akaeka setting 2mp na mwengine 8mp basi mmoja simu yake itatoa picha za kb kadhaa nyengine mb kadhaa.

ukichukua maelezo haya ukachanganya na ya dreamchaser swali lako litakuwa limejibika
 
Yaaap nashkuru sana nimeridhika na majibu....
 
uzuri wa huku angalau watu wanatumia staha kubwa ksatika kujadili hadi somo linaeleweka, shida ni kule majukwaa ya akina mwafulani
 
Inategemea na forum. ...hapa ukileta mipasho utakuwa hujitambui
 
Kwa wote mliochukua muda na kufafanua kuhusuhii mada Mungu awabariki sababu mmetuongezea ujuzi mkubwa
 
Hili jukwaa lilinifanya nijisajili jf officially baada ya kuvisit kama guest kwa zaidi ya miaka miwili
 
na kwa screenshot inakua ni nin?
 
pia kumbuka camera zinakuaga na automatic focus ambayo pia hu determine ukubwa wa picha kulingana focus ilivyoji set
 
Majibu yamenitosha sana.....
Lkn ukubwa wa picha ndo ubora wa picha.....?
 
uzuri wa huku angalau watu wanatumia staha kubwa ksatika kujadili hadi somo linaeleweka, shida ni kule majukwaa ya akina mwafulani

hili ni jukwaa la science na tech sio siasa au ubishi wa dini!!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…