Kwanini kwenye nafasi za kisiasa hakuna fair play kama ilivyo soka?

Muite

JF-Expert Member
Sep 10, 2013
2,824
6,254
Katika soka inapotokea mchezaji kaumia kunakuwa na fair play, na hata wachezaji wenyewe wanapokuwa uwanjani wanatakiwa ku balance mambo ili wasiumizane, hata waamuzi nao hutakiwa kuwa FAIR wanaposimamia mchezo.

kwenye nafasi za kisiasa:

Najua kila mtu ana haki kuteuliwa, kugombea nafasi zozote kulingana na sifa stahiki na kama mtu huyo ana uwezo au jamii inamuhitaji. mfano Rais, uwaziri, ubunge, ubalozi nk.

Lakini najiuliza ni kwanini kwenye hizi nafasi kusingewekwa mipaka au kama sio mipaka basi kuwe na uungwana/Fair Play. kwa mfano: familia moja amepatikana Rais wa nchi, ni dhahiri kwamba sio tu familia hiyo itapata ahueni kimaisha direct and indirect,ila wapo ndugu ambao hata Rais haitakuwa rais kuwakumbuka au kuwafahamu lakini wata channel kupitia yeye. watasoma, watapata kazi kirahisi, watapata mikataba kibiashara nk na hii itasambaa ktk ukoo mzima hata kucheua,hali kadhalika katika nafasi za uwaziri nk.

kama familia A imetoa Rais na hapohapo mtoto anateuliwa kuwa waziri na mwingine Mbunge wa Afrika Mashariki. Je ni kweli hakuna familia zingine zenye wasomi au sifa stahiki? pia ikumbukwe hapa kuwa baba alikuwa mkuu wa nchi hivyo bado anapewa huduma zote na serikali(ni haki kwa mujibu wa katiba). lakini hawa watoto nao kwa nafasi zao kubwa wanapewa huduma na serikali zao. FAIRNES ninayoizungumzia hapa ni kama Familia A imetoa Rais basi nafasi zingine kama uwaziri nk wapewe familia B au C ambao wana sifa pia.

Najua hii ya familia moja kupewa nafasi lipo nchi nyingi lakini kwa Africa nadhani ni zaidi.

I HOPE THE NEXT GENERATIONS WILL DEBATE ON THIS. FAIRNESS ON POLITICAL AND GOVT OCCUPATION
 
Kuna hii nayo, jimbo limepata bahati kubwa sana ya kumtoa rais wa nchi. Cha ajabu, badala nafasi mojawapo ya uwaziri ingepewa jimbo jingine, bado na mbunge wa jimbo hilohilo nae anapewa uwaziri. Bila ya kujali mnaweza shutumiwa mna njama za upendeleo na/ au ulaji mnapanga kufanya. Ndio siasa hizo.
 
Back
Top Bottom