HOMBOY
JF-Expert Member
- May 16, 2016
- 1,431
- 924
Kwako mfwatiliaji wa mabingwa wa kuchekesha wanaoishikilia rekodi ya wachekeshaji waliotazamwa sana kwenye TV nchini Tanzania kuanzia time hiyo ya Ze Comedy mpaka Orijino Komedi walivyokuwa wanawafanya watu wawahi TV zao kila Alhamisi jioni.
Ni kitambo kidogo hatujawaona Orijino Komedi kwenye TV (TBC 1) na inawezekana maswali tuliyonayo ni mengi lakini hakuna hofu tena maana tumempata Joti na amekubali kuongelea kwa ufupi.
‘Kama kundi tuna taratibu zetu na ndio maana tumejaribu kutumia muda wa mwaka mmoja kupumzika maana toka tuanze kufanya kazi hatujawahi kupumzika, tulivyopumzika pia sio kukaa kimya tukaangalia project za kila mtu binafsi na ndio maana unaona kila mtu na shughuli zake‘ – Joti
‘Ukimfatilia Mpoki kuna shughuli zake anafanya na inajulikana, Masanja pia vivyo hivyo… na mimi nimefungua Youtube channel yangu ya Joti TV, nafikiri mwaka huu tunaweza kurudi kazini pia.
Je mazungumzo ya huyu bwana mdogo yana ukweli? au baada ya huu utawala wa kiimla walipigwa stop,mpaka watakapopangiwa vyakuigiza. karibuni kwa mjadala