Kwanini jengo la DIT Teaching Tower linachukua muda mrefu hivi kumalizika kujengwa

stanleyRuta

JF-Expert Member
Jul 19, 2014
851
519
Hiki chuo inabidi kifanyiwe uchunguzi ni kwa nini hili jengo haliishi?

Nimeanza hapo masomo mpaka nikamaliza miaka minne na jengo nikaliacha hivyo hivyo nilivolikuta.

Je ni kwamba serikali haina hela ama hela imetolewa wajanja wakaitafuna, hili suala la kuchelewesha miradi kuanza kufanya kazi ilokusudiwa ni kusababisha hasara kubwa kwa kodi zetu maana hela inakuwa imelala haifanyi kazi.

Kondoro na wenzako tunaomba ufafanuzi juu ya hili maana vijana wamechoka kusomea madarasa mabovu ya T hali ya kwamba kuna mradi mkubwa wa mabilioni umelalia hela kibao.
 
hata mimi inanishangaza sana maana tokea naingia mwaka wa kwanza mpaka sasa namaliza mwaka wa tatu sioni mabadilko yeyote katika jengo na tuliambiwa "mtasomea teaching tower hivi karibuni".
 
hata mimi inanishangaza sana maana tokea naingia mwaka wa kwanza mpaka sasa namaliza mwaka wa tatu sioni mabadilko yeyote katika jengo na tuliambiwa "mtasomea teaching tower hivi karibuni".
Mkuuu si bure kuna kitu kinaendelea hapo.....
hata mimi inanishangaza sana maana tokea naingia mwaka wa kwanza mpaka sasa namaliza mwaka wa tatu sioni mabadilko yeyote katika jengo na tuliambiwa "mtasomea teaching tower hivi karibuni".
 
Hilo jengo nahisi kuna tatizo upande wa ela maana sisi tumeanza mradi mkubwa wa umoja wa vijana na mpaka umeisha lakini hilo jengo bado inadibi mpigane tochi hapo dit sio bure kuna kitu
 
DIT members inaonyesha wazi kuwa sio wafuatiliaji wa mambo yenu ya msingi, jengo ni lenu,wengine mmesoma hapo miaka 4,wengine 3,muda wote huo mnanung'unika chini chini weeeh mmeweza kuvumilia mpaka leo mmeondoka hapo ,HAMJUI NINI TATIZO! leo mnakuja hapa kwenye forum mnaendelea kunung'unika! Mnauliza maswali ambayo kipindi chote mkiwa chuoni hamkupata Majibu! Mnataka tuwapime uelewa wenu darasani kupitia thread Kama hizi sio....!?? Tuna-wasi wasi sana na watu wa namna hii, MAGUFULI KWELI TUNAKAZI YA ZIADA NA WASOMI WETU HAWA!
 
Jaaaa! Ilikuwa Safari ndefu sana toka 2005/18 hatimae jengo limeishaka limeisha kamilika na linatumika na wamenunua na gari kwa ajili Tour Study
 
Back
Top Bottom