Salvatory Mkami
Senior Member
- Apr 17, 2013
- 146
- 244
Nimejaribu kurudia kuisoma kwa umakini mkubwa Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania lakini nimeshindwa kuona mahali ambapo panatoa mwongozo au kuonyesha utaratibu wa kufuatwa pindi inapotokea chama Tawala kushindwa katika Uchaguzi Mkuu na kutakiwa kukabidhi mamlaka kwa chama cha upinzani.
Kama Katiba haionyeshi au hakuna kabisa kipendele hicho basi ni wazi kwamba haitakuwa rahisi kwa Serikali iliyoko madarakani kukabidhi madaraka kwa chama kingine chochote mbadala kwasababu Katiba haitoi mwongozo wala kuonyesha utaratibu wowote unaofafanua jambo hilo.
Mbali na mapungufu mengine ya Katiba yetu
Swali langu ni Je,
Hatuoni kwamba pungufu hilo moja ni sababu mojawapo kubwa ambayo inatoa mwanya kwa mamlaka husika iliyoshika dola kutumia nafasi hiyo kuminya demokrasia ili kuendelea kubaki madarakani kadiri itakavyowezekana?!
Katika uhalisia usio na nguo nakubali kukubaliana kwamba Katiba yetu ina mapungufu mengi sana kutokana na ukweli kwamba bado katiba yetu iko katika mfumo wa chama kimoja na si vyama vingi kama jinsi tunavyoamini, na hiyo ndio sababu kubwa iliyopelekea uhitaji wa Katiba mpya ambayo hata hivyo ilihujumiwa kwa makusudi na kundi husika kwa kujua wazi kwamba mabadiliko hayo yangeweza kuimarisha demokrasia nchini na kuweka usawa kwa vyama vyote vya siasa na kupelekea chama tawala kukosa upendeleo ambao Katiba ya sasa inautoa kwa chama kilichoko madarakani.
Ni yapi maoni yako?