Dear greetings to you.
Tusaidiane katika hili ambalo kwa namna moja ama nyingine linaweza kuwa msaada kwa baadhi ya watu, na pia kupelekea kupungua kwa usaliti na hata kuvunjika kwa ndoa za wengi.
Hivi inakuaje mtu uko na mume au mpenzi wako wa muda mrefu na mnapendana sana sana kwakweli.Ghafla inatokea unamuona mtu mwingine me/ke unajikuta unampenda sana pia, ila unajitahidi kua mwaminifu na kuamua hata iweje huwezi kumsaliti mke au mme wako,tatizo linakuja ukimuona au kumkumbuka unaanza kumpenda tena.
Tafadhali hii inawahusu zaidi wale watu wenye msimamo na mahusiano yao ambao japokua hali kama hii inawakuta hawako tayali kuwasaliti wapenzi wao hata iweje. Sema tu inawachukua muda sana kuondokana na hali hiyo ya kumpenda mtu mwingine.
Jinsi gani mtu anaweza kufanya ili hata kama akimuona amuone wa kawaida tu tafadhali wale waliozoea michepuko na watoto msilete mzaha.
Wapeni nafasi wakubwa walete busara zao hapa na kusaidia watu.