Hivi sasa UK kuna mjadala mkubwa utakao pigiwa kura za maoni 22 June 2016 kuhusu hatma ya UK katika umoja wa Ulaya. Kinacho nifurahisha, ni namna gani washiriki (wananchi kwa vyama mbalimblai) mjadala huu hawana upande kwa mtizamo wa kichama au itikadi. Kwa mfano Waziri Mkuu Cameron, baada ya kuamini kapata "deal" anashawishi wananchi wapigie kubakia, wakati baadhi ya mawaziri wake na hata Meya wa jiji la London Boris Johnson (mwanasiasa anaye pendwa ndani ya chama chao na hata anazungumzwa kumridhi Cameron), yupo kambi tofauti ya kutoka.
Nyumbani ni vigumu kukuta kuna hata mwanachama wa CCM, achilia mbali viongozi wanapingana kwa wananvyo amini wao (ukiachana na wachache baada ya kuwa sio viongozi tena kama Moyo na Kaduna) lazima iwe sawa wasemavyo viongozi. Hili lina mchango mkubwa wa kutofanikiwa kwetu maana kutofautiana mawazo na misimamo ya watu hupelekea kufanyika kwa maamuzi sahihi na kuharakisha maendeleo. Na naamini kabisa hili lingefanyika, suala la Zanzibar lingekuwa historia na hivi sasa tungekuwa tunashghulikia masuala mengine muhimu sana ya kimaendeleo, sio kjikuta katika mgogoro ambao kwa dalili zote hata uchauzi ufanyike ndio kwanza mwanzo wa migogoro na maendeleo ya kweli kwetu kubakia ndotu tu.