Pole mkuu kwa msoto wa hasara lakini hata mimi ningekuwa baba yako nisingeweza kurisk biashara kwa kuweka mtu mwenye historia yako ya kufeli na kumtoa mtu ambae kwenye vitabu kazi yake inaonekana, prove yourself kwanza na mzee atakuamini. Kuhusu pesa hizo ni dalili mbaya, kama chini ya uangalizi unaweza kuficha, vipi ukikabidhiwa?
Umeongea ukweli mkuu, hakuna alie mwaminifu kwa namna yoyote ile ukiwa umeajiri faida unaiona na maendeleo unayaona hutaangalia mfanyakazi anapata nini bali wewe unapata nini.Hakuna wizi mkubwa wala wizi mdogo. Mwizi ni mwizi tu mkuu.
Hapo nafikiri baba yako anawaamini hao vijana kwasababu ndio walio muwezesha kufikia hapo alipo, na inawezekan hata mzee wako pia hatazami wao wanaiba nini zaidi ya kuangalia yeye anapata nini.
Minafikiri mzee wako yupo sahihi kwasababu anaiona faida, hata kama wanamuibia.
Kweli mkuu, ilitakiwa huyu amfanye kua rafiki ake na ampende na kumuomba ushauri na hata kama amejua mzee wake anapigwa angemezea pengine ungekuta na yeye anapata gawio kidogo toka kwa muuzaji, tatizo lake yeye alifika ofisini na kujifanya kaja kumsaidia baba ake kulinda hesabu na sio kufanya kazi kama wafanyakazi wengine.Kama mzee wako ana muamini huyo kijana usiumie, jitahidi uwe mpole na mnyenyekevu huku ukijifunza. Kama umeweza kwenda porini na kupambana nina imani utaweza kufungua biashara yako mwenyewe.
Tazama miradi na biashara ya mzee wako kwa kujifunza, mpende sana huyo jamaa usimchukie atakusaidia sana.
Usimdanganye kijana, hapo hakuna la kuongea na baba yake zaidi ya yeye mwenyewe kubadilika ili aendane na biashara ya baba yake pamoja na wajakazi alio wakuta.Ongea baba yako vizuri muyaweke sawa.
Ila hapo unakomazwa ndugu yangu.
Endelea kukomaa ili mafanikio yako yawe imara
Minaona kama wewe ndie haujielewi, maana hapa umekuja na simulizi za kwamba waajkazi wanamuibia mzee. Na naona kama unaumizwa na wivu wa wajakazi wa babayako kufanya maendeleo.Ni kweli hakuna wizi mdogo wala mkubwa ,inakuwaje sasa mwizi anapata nguvu ya kwenda kumsemea mwizi mwenzake ili afukuzwe abaki yeye !
Mzee analalamika sana , kuhusu maendeleo ya ofisi zake.