Heshima yako Mbuzimtu, pia nikupe pole kwa kilio ulichokitoa cha kukosa kuona ziara za viongozi wetu CDM kitaifa.
Ni ukweli usiopingika, ujio wa viongozi wa kitaifa ni faraja kubwa kwa wapiga kura hawa watarajiwa ktk kuchagua diwani, mbunge na rais kupitia UKAWA.
Niungane na wewe kuwaomba viongozi wa kitaifa kufika majimbo haya: Ileje na Rungwe Mashariki (BUSOKELO). Kilio cha wananchi hawa kutopata ziara ya viongozi wakuu kitaifa kimekuwa sugu. Na ni majimbo ambayo wananchi wake wako tayari sana kwa mabadiliko km ilivyo Kyela, Mbeya Mjini n.k
Mwisho nishauri, wabunge wa CDM ni aseti kubwa kwa chama wajitahidi kutoka na kufanya ziara kwa kushambulia. Majimbo mengi tutayachukua uchaguzi ujao lakini jitihada iongezeke kidogo, japo changamoto inaweza kuwa fedha hata hvyo wananchi wako tayari kuchanga kuwezesha ziara za waheshimiwa wabunge na viongozi wakuu wa chama. Kikubwa ni utayari tu makamanda.