Allen Kilewella
JF-Expert Member
- Sep 30, 2011
- 20,353
- 38,559
Jengo la Ofisi ndogo ya CCM iliyoko Mtaa wa Lumumba
Kati ya vyama vyote vya siasa vilivyopo Tanzania,CCM ndiyo chama kinachoongoza kwa kuwa na Utajiri Mkubwa sana wa Rasirimali vitu. CCM ndiyo yenye majengo Mengi (Kihalali na si kihalali) na ndicho chama kinachomiliki viwanja vingi kuliko chama kingine chochote kile! Na kwa nasibu pia ndiyo kimetokea kuwa chama kinachoongoza nchi hii kwa miaka mingi sana.
Lakini kinachoshangaza ni kwamba wananchi wanaoongozwa na CCM wengi wao wanaishi kwenye umaskini na ufukara uliotukuka.Sielewi ni kwa nini chama chenye ukwasi wa kiasi hiki kinashindwa vipi kutumia mbinu zilizokipa ukwasi wa kiasi hicho kubadili hali za wananchi kinaowaongoza.
Wakati mwingine utakuta mwana CCM anayesifia ukwasi wa chama chake dhidi ya CHADEMA kwa mfano, yeye mwenyewe hana uwezo wa kusomesha mwanawe hadi ada ya shilingi 20,000 kuondolewa kwake alishangalia, hana maji safi na salama, hana uwezo wa kulisha familia yake kwa uhakika, hawezi kujitibia hospitalini aumwapo na mengine mengi yanayodhihirisha umaskini na ufukara alionao.
Kwa kila hali inaonesha kwamba CCM ni tajiri sana lakini watanzania wengi ni maskini na miongoni mwao wamo wale wanaojitapa na kujigamba kwa utajiri wa chama chao CCM. Ni nini kinazuia chama hicho tajiri kuwafanya wafuasi wake na watanzania kwa ujumla kuwa tajiri kama chenyewe kilivyo?
Nyumba mojawapo ya Mtanzania anayeishi kwenye nchi inayotawaliwa na CCM, chama cha siasa tajiri kuliko vingine vyote vilivyoko Tanzania.