Mwanahabari Huru
JF-Expert Member
- Mar 9, 2015
- 14,243
- 34,903
Kura za maoni za uwakilishi na udiwani ndani ya Chama cha Mapinduzi Zanzibar ili kupata wagombea kwenye Uchaguzi Mkuu Oktoba 2015 zilifanyika mapema mwaka jana, na wagombea walipatikana. Aidha mgombea wa urais CCM alipatikana pia.
Lakini pia historia inaonyesha kwamba katika chaguzi zote zilizopita vyama pekee vinavyoshinda kwenye nafasi zote za urais, uwakilishi na udiwani huko Zanzibar ni CCM na CUF pekee. Maana yake ni kwamba kama moja kati ya vyama hivyo viwili hakishiriki uchaguzi basi kingine ni kama kinashinda bila kupingwa.
Kwa kuwa Chama cha Wananchi CUF kimetangaza kutoshiriki uchaguzi wa marudio wa tarehe 20/03/2016 ni kama CCM imeshashinda nafazi zote za urais, uwakilishi na udiwani - kwa maana ya wale waliopitishwa kwenye kura za maoni. Kwa hiyo tarehe 20/03/2016 ni kama kufanya uchaguzi kwa wale wale waliokwishapita kwenye kura za maoni za CCM, wakiwa peke yao.
Ndiyo maana najiuliza kwanini CCM wanataka kurudia kura za maoni tarehe 20/03/2016, tena kwa kutumia mabilioni ya fedha za wananchi?
Kwanini wasiwatangaze tu hawa makada waliokwishashinda kura za maoni kwamba ndio rais, wawakilishi na madiwani ili kuokoa mabilioni ya fedha ambazo zingetosha kuboresha hospitali, zahanati na shule za wananchi?
Dr. Milton Makongoro Mahanga