Kwanini Afrika ni masikini?

Hizb Tahrir Tanzania

JF-Expert Member
Joined
Feb 18, 2020
Posts
258
Reaction score
235
Duniani kuna aina za nchi kulingana na mfumo, nguvu zake kiuchumi, kijeshi na kisiasa:

1. Super powers
Hizi ni nchi zinazoitawala dunia. Ndiyo zinashikilia mfumo unaoendesha dunia (ideology) Ndani yake kuna taifa kiongozi (leading nation) ambayo kwa hali ya sasa mfumo Ni Ubepari (capitalism), superpowers ni nchi kama Amerika, China, Urusi, Ujerumani, na taifa kiongozi ni Amerika

2. Independent States
Hizi ni nchi huru ambazo zinaweza kuamua sera zake zenyewe bila kulazimishwa na superpowers. Hizi huwa nchi zenye uwezo pia. Nchi kama Sweden, Denmark, Switzerland zinaingia hapa

3. Subordinate States
Hizi ni nchi zinazokoloniwa, hazina sera binafsi bali sera zake ni sera za mkoloni wa muda huo. Nyingi ni nchi masikini za Afrika na zinazoendelea. Wakoloni hupanga chama cha kutawala, muda wa kutawala, na nani atawale,nk

Afrika inaingia kwenye hili kundi la tatu hivyo haina mfumo, haina uhuru, haina nguvu za kijeshi, kiuchumi, wala kisiasa na kwahiyo inabaki kuwa masikini
 
Socialism ( everybody is equal ) it will never work
 
Wapinzani wanachangia Africa kuwa maskini Kwasababu wanatumika na Mabeberu kuharibu Amani na utulivu wa Nchi za kiafrica
 
... tumehabarishwa sana jambo hili. Kwamba, ili nchi iendelee inahitaji vitu vinne vya msingi yaani ARDHI, WATU, SIASA SAFI, na UONGOZI BORA. Katika manne hayo, dadavua mwenyewe Afrika inakwama wapi.
 
... tumehabarishwa sana jambo hili. Kwamba, ili nchi iendelee inahitaji vitu vinne vya msingi yaani ARDHI, WATU, SIASA SAFI, na UONGOZI BORA. Katika manne hayo, dadavua mwenyewe Afrika inakwama wapi.
Uongozi bora, huwezi kuwa na viongozi wenye mawazo mgando kama jiwe na bashite na Ndugai utegemee maendeleo ndani ya nchi yako.
 
Uongozi bora, huwezi kuwa na viongozi wenye mawazo mgando kama jiwe na bashite na Ndugai utegemee maendeleo ndani ya nchi yako.
Kama taifa lina watu wenye mawazo mgando hivyo ni lazima hata viongozi wake wawe wenye mawazo mgando maana,haiwezekani tukawa tunapata viongozi waliyo tofauti na sisi tulivyo.
 
Kama taifa lina watu wenye mawazo mgando hivyo ni lazima hata viongozi wake wawe wenye mawazo mgando maana,haiwezekani tukawa tunapata viongozi waliyo tofauti na sisi tulivyo.
Dah ukweli mchungu huu.
 
Democracy zitatugawa ichi maskini......mabebebru wanapitia vyama pinzani kutuendesha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…