Kwangu ndoa haitokuwa ndoano kamwe!

Kashindi

JF-Expert Member
Joined
Oct 28, 2011
Posts
349
Reaction score
250
Sitapenda, sitafurahi na sitopendezwa mke wangu kuvumilia tabia zangu za ajabu ajabu zinazomkosesha raha, kumvunjia heshima na zenye kumuumiza mara kwa mara kwenye ndoa eti kisa anataka kulea watoto na kujenga ndoa yake.

Sitokuwa tayari kumvumilia tabia zake za ajabu ajabu atakaye kuwa mke wangu zenye kuniumiza, kunikosesha raha na amani katika maisha yangu eti kisa nataka kujenga ndoa na kulea watoto.

Ni jukumu letu sote kuhakikisha kila mmoja wetu anakuwa na amani, furaha, na utulivu wa nafsi, utu, heshima na utulivu wa nafsi ni jambo la kuzingatia kwenye ndoa.

Kwangu mimi sipendi ndoa iwe kitanzi kwa mke wangu au kwangu mwenyewe. Nikishindwa natoka. Nitakuwa huru siku zote za maisha yangu, nitailinda furaha yangu na ya atakaye kuwa mke wangu. Ni jukumu letu kama wazazi kuhakikisha kuwa watoto tutakaowazaa wanakuwa wenye amani, furaha, afya na upendo daima.

Kwangu mimi ndoa haitokuwa ndoano kwa sababu siko chini ya dini, maneno ya watu. Sitokuwa tayari kuyasikiliza wala kuyafuata maandiko yanayosema eti kuachana na mke wangu ni dhambi. Mimi ni kiumbe huru.

Mwalimu Msomi Kashindi Emanuel
 
mmmmmh hutaki kujikera nafsi kisa watoto lazima walelewe na Baba na Mama...
 
[emoji145]
[emoji23]
[emoji153][emoji106]nice
[emoji158]
 
mmmmmh hutaki kujikera nafsi kisa watoto lazima walelewe na Baba na Mama...
sio lazima hasa pale inaposhindikana baba na mama kukaa na kujenga pamoja. alway a canoe cannot move if everyone sails on his own. kama hakuna maridhiano hakuna haja ya kusema uvumilie. njia za kulea watoto zipo hata kama hampo pamoja.
 
sio lazima hasa pale inaposhindikana baba na mama kukaa na kujenga pamoja. alway a canoe cannot move if everyone sails on his own. kama hakuna maridhiano hakuna haja ya kusema uvumilie. njia za kulea watoto zipo hata kama hampo pamoja.
Raha ya watoto nikulelewa na Baba na Mama sasa mama akivumilia hua nzuri zaidi manake Baba uvumilivu hua mdogo sana.
 
Safi sana.. you become what you wish for.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…