Kwako wewe mwanamke

Rohombaya

JF-Expert Member
Joined
Jul 4, 2011
Posts
13,082
Reaction score
10,443
Sihitaji kujua hali yako,Uliponipigia Simu na kunitajia hii ID yangu ndiyo kumenisukuma kuandika haya.
Nilikutana na wewe ukipata dinner kwenye Chinese restaurant Barabara ya samora ukiwa mwaka wa pili tu chuoni pale karibu yake, nikavutiwa nawe.

Nikakupenda, nikakuthamini, nikakuamini...kumbuka over the first 3 months sikuweza kusex nawe kwani nilikuona uko so sweet n clean kiasi nikahisi kama nitakuchafua hivi japo tulikuwa na privacy za kutosha. Ninashukuru kuwa miaka 4 ya amani na furaha nimepata hawa boys wawili kupitia kwako.

Nilikuwa muwazi sana kwako ( may be this was the first mistake) kuwa kukushirikisha kila kitu changu. Nilihakikisha natimiza wajibu Wangu kwako ili kukufanya uwe na furaha wakati wrote. Nilikueleza wazi I wasn't happy with my employment na ninataka kuquit wewe ukakataa japo nilikueleza kuwa Mimi ndiyo nafanya kazi lakini wazungu ndiyo wanapokea malipo ukaniuliza wapi nitalipwa kama vile sikukujibu.

Wiki moja baadaye niliamua kuachana na wale wazungu, ninakumbumbuka nilirudi nyumbani jioni siku ile nilivyokueleza ulikasirika sana ukawa kama mnyama, ukaninyima haki yangu usiku ule na kibaya zaidi ukagoma kuwanyonyesha watoto nakumbuka walilia usiku kucha hiki nikihangaika kuwapa maziwa ya kopo.Tokea hapo haukutaka tena mawasiliano nami japo hili halikunisumbua kama ulivyokosa mud a na watoto wakati Mimi ninajipanga kwa maisha mapya.

Siku ya tano to kea niache kazi haukurudi nilikupigia Simu Mara nyingi na ukawa unaikata nikampigia sis wako nikamueleza baadaye ukanitumia text kwamba uko poa nami nilee watoto. Ninamshukuru yule dada kwani siku 2 nilishinda ndani nawahudumia wale malaika wa miezi10 had I yeye aliponiambia kuwa upole "shemeji nenda kazini nitawaangalia hawa watoto" kidogo machozi yanitoke Ila niliweka ahadi moyoni.

Maisha yaliendelea vizuri bila wewe, na watoto ni wakubwa na HAWAKUJUI wanajua mama yao ni yule dada uliye muacha, na sikuwaambia hili Bali niliona wameandika jina la huyu dada kama mama yao katika majibu ya mtihani wao miaka2 iliyopita..I was happy.Umezunguka mabara yote duniani sijui ukifanya ni ni kuwa miaka yote hiki na Leo watoto wamekuwa wakubwa na Mimi nimeingia kwenye reli ya kwenda to my dreams unakuja eti u need a second chance ya ni ni? Wakati we live only once.

Na usijaribu hata kwenda kuwaona watoto shule watakuona chizi ukiwaambia wewe ni mama yao kwani huyu dada anawafanyia mengi na anawapenda na wao wanampenda tena kuliko Mimi.Nimeyandika hata bila uchungu wowote moyoni, na kama ningeijua ID yako basi ningekuPM ili uwe unarudiarudia kusoma labda utaelewa kwamba Mimi nawe tena will never happen na kama ulivyosema kuwa you can't live without me hapo ninaweza kukupa Pesa kidogo utafute short cut ya kutoishi. Ila nisahau Mimi na watoto
 
Hekaya yako imekaa vizuri isipokuwa "timeline" na matukio vyatia shaka...
 
Kuna watu wana roho za kutu...wanao mwenyewe ukatae kuwanyonyesha dah inasikitisha akiwadhulumu hao malaika haki zao for what?Huyo mwanamke ni katili na hastahiki kuitwa mama...Pole sana mheshimiwa!!
 
Hekaya yako imekaa vizuri isipokuwa "timeline" na matukio vyatia shaka...

Nilidhani nimeona hili peke yangu. Mara miaka minne, mara watoto wapo Shule na Wanajua kuandika jina la mama yao

Mara kaacha kazi na Baada ya siku mbili anasaidiwa watoto na kuambiwa aende kazini
 
Najua ulikuwa unakatisha matukio ktk kuandika.

Mkuu mimi wazo langu ni kwamba huyu mtu hakufai ktk maisha maana ni katili sana kama baba yake shetani.

Release her in your heart but dont dare to give her a second chance.
 
Hongera (kwa kwa kwa kwaaa)
Imara (kwa kwa kwa kwaa)
Waaa (kwa kwa Kwa kwaaaaa)
 
Najua ulikuwa unakatisha matukio ktk kuandika.

Mkuu mimi wazo langu ni kwamba huyu mtu hakufai ktk maisha maana ni katili sana kama baba yake shetani.

Release her in your heart but dont dare to give her a second chance.
Hunyu hivi kile kichaa kilipona? Ulitoka lini milembe kule dodoma?
 
Last edited by a moderator:
kuna watu hawafai kuoa mkuu..na pia kuna watu wapo unstable sana challenge kidogo tu shida mpaka basi
 
Kutendwa mwisho Mara moja in lifetime...
 
Sijambo, kwanini umekuja kunianika hapa jf, kwani tulikutana hapa????????????? leo nakuja kubeba watoto wangu na huyo dada unayejivunia naondoka nae, sawa?????
Mamaaa wee dnt tell me u r M**** kwani nitazimia....please
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…