Kwako mkuu wa mkoa wa Dar Es Salaam

kombaME

JF-Expert Member
Aug 24, 2015
2,115
2,815
Mkuu kwa kuwa umeonesha nia ya dhati ya kupambana na tabia mbaya na uvunjaji wa utamaduni wetu kama ushoga,basi mimi nakukumbusha kuna tabia zingine nyingi ambazo zinafanana na hizo ambazo sio tamaduni zetu na hazifai kuachwa maana zitaigwa na watoto wetu,pia hii itaondoa malalamiko kuwa unaona upande mmoja, baadhi ni...

1.uvaaji wa vimini,
mkuu ukiachana na sababu kwamba watoto wetu wataiga hii tabia ila pia ni chanzo cha tamaa ya ngono na kupelekea maambukizi ya UKIMWI kuwa juu

2.Milegezo
Hii sasa ni tatizo mkuu usiwaonee mashoga tu angalia na hili

3.Kujichubua
Mkuu hii inapelekea kansa, twende nao sambamba

Kwa leo niishie hapa ila mkuu angalia pia ratiba yako ya mwaka usije ukajikuta unapigana na vitu ambavyo havileti umeme,maji, miundo mbinu wala elimu bora. Kila la heri
 
Back
Top Bottom