Kwako Kaka yangu ,Albert Msando

chuo kikuu ndiko ulikoenda kufundishwa kuandika hizi riwaya?
 
Tuna viongozi wanaosaka sifa na si kutatua matatizo ya wananchi!!!
 
Ushapata ajira mkuu?.
Naona umepata bando la kuja kutusumbua huku.
Wewe ambaye sio kalunguyeye umemsaidia nani?/ au hauna cheo na wewe tafuta kiki jina likuwe maana na msando naye lilikuwa lengo lake.
 
Msando msanii na ametumia fursa vizuri hiyo milioni tano itampa mabilioni muda siyo mrefu
 
Kwanini umpangie mtu chakuwaza?
 
Jamani mwenye mawasiliano ya Kaka Msando anisaidie pengine aweza nisaidia na mie raia niliye chini ya rais mpendwa.

Asante
 
Dogo ana uwezo sana badala ya wahusika kumuona adui wanatakiwa kuanza kumjenga katika nafasi za serikari ya miaka 20 ijayo.

Mabeberu ya miaka 20 ijayo na yenyewe yatakuwa na werevu zaidi kushinda ya leo kuichallenge inataka watu wenye uwezo.

Let’s face it kwa TISS ya leo ukilinganisha na wenzetu kwenye mambo ya maslahi ya taifa ni ovyo bado wapo defensive badala ya kuwa wabunifu. You need clever people to do that job and this kid looks the part.
 
Ni upuuz kuwaza kua Albert anaweza saidia “Jamii kwa mapana”(sijui hata huyu dogo anamaanisha nini since idadi ya watu ambao anasaidia ni kubwa mno ku affect jamii nzima).
Msando kafanya sehemu yake,wewe Kalukalanga umefanya nini ndo swali.Usiwe tu unatoa changamoto sababu huamini anachoamini yeye kwenye siasa...
 
Mida mingine serikali inapoteza hela kuwasomesha watoto kama hawa, bora hela zingeelekezwa kwenye tafiti ambazo zinatija kuliko kudhamini vichwa kama hivi.
 
Wewe zwazwa unaemuiga Zitto kwani umekatazwa kwenda kutoa msaada na wewe. Alafu embu mfuatilie huyo Msando kama huyu ndie mtu wa kwanza kumsaidia. Wivu mwingine wa kipuuzi sana. Kinachowauma ni nini na mtu katumia pesa yake? Tabia za kike hizo mpaka tunaanza kupata shaka na wewe, tabia zako hazina tofauti na Suphian yule wa Twitter
 
Umeandika vyema kwamba wapo waliopaswa kutatua changamoto kama hii aliyokutana nayo Mh.Rais lakini wameshindwa kufanya inavyostahili, hata mimi nilishangazwa na kusikitishwa sana kuona hali hiyo nilijiuliza hivi maprofesa wote hao hapo muhimbili na wasomi wote wameshindwa kabisa kubuni namna ya kukabiliana na tatizo kama hili sababu sidhani ni mara ya kwanza inatokea, yaani wao hawana habari na uwezo wa waangalizi wa wagonjwa wao kiuchumi..kama wataweza kumudu gharama za matibabu ya mgonjwa wao???kama wanadhani si jukumu lao basi hata huduma yao si ile inatoka moyoni kusaidia watu! walipaswa wajue mambo haya, mgonjwa anapolazwa hospitalini kwao wanapaswa kuwa na details zote si za ugonjwa tu, hata background ya mgojwa kijamii na kiuchumi..anatoka wapi, nani amemleta, anajishughulisha na nini, nani wanamhudumia akiwa nyumbani nk, haya nayo ni sehemu ya tiba! Nitoe ushauri hata kwa msando, ipo hospitali moja sitaitaja kwa jina wao wana kitu kinaitwa Hospital Bed Fund..ni mfuko wa kusaidia gharama za matibabu kwa wale wote wanakuwa na vigezo vya kusaidiwa pale inapohitajika, ni mfuko unachangiwa na watu wote wakati wowote, hospitali inausimamia kiuendeshaji na kwa kweli unasaidia sana kupunguza makali ya kuuguliwa muda mrefu na hata pale mgonjwa inapotokea amefariki..Msando asiishie hapo vile amejitolea kumsaidia Mh. Rais kwa jukumu hili.
 
Hizi ni kanuni za njia.

1. Kusaidia jamii nzima ipate suluhu ya suala la afya ni bora kuliko kumsaidia mtu mmoja mmoja.

2. Kumsaidia mtu mmoja ni bora kuliko kutosaidia hata mtu mmoja.

3. Kutomsaidia mtu hata mmoja ni bora kuliko kumhatarisha mtu mmoja

4. Kumhatarisha mtu yeyote si bora zaidi ya kuhatarisha wengi

5.Kuonesha kitu kizuri zaidi kwa vitendo ni bora kuliko kusema maneno

6. Kumsifia anayefanya vizuri ni bora zaidi ya kukaa kimya

7. Kukaa kimya ni bora zaidi ya kumvunja moyo anayefanya vizuri

8.Kutoa bila matangazo ni bora zaidi ya kutoa kwa matangazo

9. Kutoa kwa matangazo ni bora zaidi ya kutotoa

10 Kutotoa ni bora zaidi ya kubadhiri cha muhitaji
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…