jang
JF-Expert Member
- Jul 31, 2014
- 1,413
- 1,180
ANGALIZO KWA RAIS WA TFF JUU YA HAYA YANAYOENDELEA KUHUSU SIMBA.
''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''
Imeandikwa na
Said Ngulipa
Kwanza kabisa nakupa pole na majukum ya kuusogeza mpira wetu mbele na nitakua mchoyo wa fadhila kama sitakupongeza kwa jitihada zako za kututengenezea tm ya vijana (Serengeti boys) iliyo bora kabisa kuliko zote zilizopita kwa miaka ya karibuni.
Mh, Rais wa TFF, bila shaka ww ndo mhusika mkuu ktk sifa zote na lawama zote zinazotokea kwenye shirikisho letu la mpira wa miguu,
Kwa point hyo ni wazi kwamba unahusika ktk kila kinachoendelea kwenye shirikisho bila kujali ulikaa kwenye kupitisha huo mpango au hayo maamuzi ama n.k
Tangu ulipoingia madarakani imeonekana tm ya simba imejiwekea ufalme kwamba kila inapotokea sintofaham ambayo italazim maamuzi yake yatolewe na kamati aidha ya masaa 72 au nyinginezo ni lazima washinde kama wanahitaji kushinda wkt kwa wengine hilo swala halipo, na pia wana uwezo wa kufanya kosa na wasiadhibiwe wkt wengine hawana hyo bahati.
Wadau wa mpira wa miguu wanapata mashaka kutoka na baadhi ya mambo ambayo yameonyesha ukaribu usio wa kawaida kati yako ww Mh na viongozi wa simba na hasa pale mlipokaa kikao kisicho rasmi na ukasema mlikua mnapata chakula na kubadilishana mawazo pamoja na viongozi wa simba na hatujaona muendelezo wa hvyo vikao na viongozi wa tm zingine,
Why ilikua simba tu?
Nitatoa mifano michache inayokwenda sambamba na mashaka ya wadau kuhusu huo ukaribu bila kujali hayo matukio yalitokea kabla au baada ya kile kikao ambacho mm nakiita sio rasmi.
KADI TATU ZA IBRAHIM AJIBU
Hapa tuliambiwa kuna kikao kilikaa kikaamua kwamba mchezaji atakaepewa card tatu za njano ataruhusiwa kuchagua mechi ya kuitumikia adhabu yake kati ya mechi tatu zilizo mbele yake na vilabu vilipewa barua, lakini ukweli ni kwamba hakuna club yoyote ambayo ilipewa hyo barua inamaana kiliundwa kipengere cha dharula ili kuibeba simba na kweli ilibebwa.
WACHEZAJI KUCHEZA BILA VIBALI
Ndanda waliwakatia rufaa wachezaji wa simba kwa kucheza bila vibali na baadae ikafahamika kwamba kumbe hata kocha nae hakua na hvyo vibali vyote viwili kwa maana ya
Kibali cha kuingia nchini na kile cha kufanya kazi nchini lakini haraka sana TFF ikatoa jibu kwamba hata kama hawana hvyo vibali lakini simba hawawezi kupokwa point kwa sababu hakuna kanuni inayosema hvyo.
Hii ni mbeleko nyingine kwa mkubwa.
KUFUNGIWA KWA WENGINE
Kuna kiongozi wa club moja alifungiwa kwa muda wa mwaka mmoja na TFF kwa sababu walizodai kwamba alitoa kauli zakichochezi,
Sijui ni kauli ipi ila kuna kauli ilitolewa na kiongozi wa simba kwenye mechi baina ya Azam na Yanga nanukuu "Hao wanaocheza hyo mechi ni wake zetu ni mke mdogo na mke mkubwa" ktk hali ya kawaida hutegemei kusikia mwanaume anwita mwanaume mwenzake mke wangu na nilitegemea TFF wangemwita angalau wakamhoji na kumuonya lakini hakikufanyika chochote nadhani ni kwa vile nae ni kiongozi wa simba.
KUPITIA MLANGO USIO RASMI
Kwenye hili tm zimekatwa sana 500,000/ lakini simba walifanya kosa kama hilo kwenye mechi yao iliyofanyika songea dhidi ya maji maji lakini hakuna adhabu yoyote waliyopewa.
Huyu Banda ambae kamati ya masaa 72 imetangaza kumsimamisha jana hili sio kosa lake la kwanza ameshafanya hvyo mara nyingi na alikua anafanya akijua kabisa hawezi kuchukuliwa hatua zozote
Alishawahi kumpiga ngumi Said Makapu wa Yanga na hakufanywa chochote alitakiwa aadhibiwe adhabu ijukikane kusema tu amesimamishwa asicheze mechi dhidi ya mbao haitoshi.
RUFAA YA POLICE DAR
Hapa ndo simba walidhihirisha kwamba wao ni wakubwa kuliko TFF na Bodi ya lg,
Novat Lufunga ni dhahiri alikua na card nyekundu aliyopewa kwenye mechi ya mwisho ya simba msimu uliopita kwenye FA hakupaswa kucheza mechi ya kwanza ya simba kwenye kombe la FA msimu huu.
Kama sio ufalme wao waliojipachika leo hii simba wasingekuepo kwenye FA lakini sheria ziliachwa mbali kabisa na kuwaonea police tena bila ufafanuzi wa maana eti tunaambiwa hawakulipia ghalama ya rufaa mara tunaambiwa walipeleka rufaa nje ya muda wkt ki uhalisia swala la card halina ulazima wa kukatiwa rufaa na club hyo ni kazi ya TFF rufaa ni ziada tu.
SWALA LA RUFAA YA SIMBA DHID YA KAGERA
Naona kabisa kuna mazingira yanaandaliwa ili simba abebwe tena kwa mara nyingine.
Kamati ya masaa 72 ipo chini ya Bodi ya lg na wasimamizi wa mechi wapo chini ya Bodi ya lg, inamaana ripoti zote za mchezo kuanzia ya refa wa kati na kamisaa zipo Bodi ya lg ni swala tu la kuzichomoa ripoti za mechi husika na kuzipitia cha ajabu eti leo tunaambiwa unakusanywa ushahidi zaid, sawa mechi haikuonyeshwa live na Azam tv lakini je, haikua recorded?
na kama haikua recorded ni ushahidi gn unatafutwa ambao utakua zaid ya hzo riport?
Mazingira yanaonyesha simba inataka kubebwa kwa mara nyingine.
Nikiangalia ratiba inanionyesha simba atamaliza mechi zake za kanda ya ziwa tarehe 12/4/2017 na kwa mujibu wa kamati inasema itatoa majibu Alhamisi ambayo itakua tarehe 13/4/2017 inamana kamati inasubiri ione simba itavuna nn mwanza na wanachohitaji wao ni kuona simba inashinda mechi zote mwanza ili wakiwapa na hzo point za Kagera wawe juu ya msimamo kwa point nyingi na ninaamini endapo simba asiposhinda mechi zote mwanza hata hz point hatopewa kwa maana watakua wanatwanga maji kwa kubeba lawama kwa tm ambayo hata ibebwe haitachukua ubingwa, kwa sababu wameshajua simba hawana haki ya kupewa point zile kwa maana Fakhi hana card 3 za njano kwenye vpl bali ana card mbili kwenye vpl na moja kwenye ASFC.
Mwisho
Tunakuomba mh, ziangalie kwa jicho pana hzo kamati zako
Kama wanafuata maelekezo yako sawa kwa vile umeamua mwenyewe ila kama sio kwa maelekezo yako ujue wanakuharibia kwa vile huwezi kukwepa lawama na pia hatutegemei Kagera suger anyang'anywe point.
Ahsante.