Kwaheri Mbowe katika CHADEMA

teh teh.Hii mipango ya kipuuzi,inakaribia mwisho.Mabenki hayatoi hela na mmefulia,mtapata wapi hela za kuhonga wenye njaa kama akina mzee wa kuzimu(hadi mende watakufa)
 
Mbowe tumemchoka mbowe dikteta huyu bwana anaharibu chama.kwa kwel anakula pesa za ruzuku hakuna ofisi imara mali za chama anafanya kaze...mbowe ni fisi
Wewe M-CCM Mbowe hakuhusu
 
Mbowe akistaafu nafasi ya mwenyekiti nitampongeza sana

Ni wakati wa damu mpya sasa si mbowe wala Lowassa...

Mbowe Kazi aliyoifanya ni kubwa anatakiwa pia kupumzika maana hata imemsababishia misuko suko mingi....
Mbowe hatathubutu kustaafu ili ajimalize kabisa?madeni yote aliokuwa nayo hamumuonei huruma?Uenyekiti ndio sehemu pekee iliobaki kwa hus survival!
 
Ni muda wa chama kusonga mbele sasa, huenda ruzuku ikafika na huku mashinani tujenge ofisi.

Kubwa alilofanya Mbowe ndani ya Chadema ni hamasa kwa vijana na kuwaweka wote kwenye kapu moja.

Maamuzi mabovu ambayo Mbowe hatakuja kuyasahau ni kumkaribisha Lowasa ndani ya Chadema.

Naamini hili swala hata yeye linamuumiza sana.
 
Kweli maana anadhan anawaongoza chekechea
 
Anaachaje biashara yake chini ya SACCOS ya familia. Maana Mbowe kaoa kwa Mtei,na Mtei ndio mwasisi wa chama. Afu alipe deni huyo bwana.
 
Hivi kwa nini ccm hawataki Mbowe awe mwenyekiti chadema kama dhaifu si ndio vizuri kwao
Unajua nini? Ni kuwa Mbowe amekuwa mbunifu, mjanja wa kutegua mitego ya wabaya wa CHADEMA, kwa ufupi ni strategic man! Sasa utaona tangu ameingia kuna mafanikio mengi yamepataikana hadi kutishia uhai wa CCM, historia ya 2015 haitasahaurika ktk chama cha mapinduzi, ilimanusura!

Ingekuwa inawezekana, najua wapo watakao pinga na kulaani vibaya sana, Mbowe angeendelea kuwa Mwenyekiti kwa vipindi vingine vijavyo kama vine. CCM watahar...ha wakiona ikifanyika hivyo. Mbowe, kamatia hapo hapo, kamatia chini....
 
aende tu maana hata ofisi ya makao makuu kashindwa kujenga kazi kuanzisha operations ambazo wanakula hela tu na hazina manufaa
Ameshaandaliwa Mchagga wa kushika Cheo cha Mbowe?
 


Naona CCM na CHADEMA wameungana baadhi ya maeneo
 
Hatukubali kabisa mbowe kutoka kwenye uenyekiti
 
Vizuri sana kwa uchambuzi embu chambua kama karanga na chama chako kinavyoendesha mambo ya jumla! Maana umepinda mgongo kutafuta story kwa chama ambacho hakina hata dola wakati kuna wengine wanakuntunza na kukutunza wakifanya zaidi ya hayo unayoyaeleza! Embu elezea tuone umahiri wako!
 
Mbowe akistaafu nafasi ya mwenyekiti nitampongeza sana

Ni wakati wa damu mpya sasa si mbowe wala Lowassa...

Mbowe Kazi aliyoifanya ni kubwa anatakiwa pia kupumzika maana hata imemsababishia misuko suko mingi....
Mbowe akiachia nafasi ya mwenyekiti usishangae akabadili gear kama kiongozi wa UKIP Nigel farage akarudi tena. Tatizo anaowaongoza wanadhani hawawezi kudumu bila yeye ona hata hapa comments zinavyojionyesha kila anayeunga mkono kuachia ngazi kwa Mbowe hata kama siyo mwana ccm anapewa jina la ccm. Hili Taifa haliwezi kuendelea mbele maana limejaa raia mbumbumbu na wanasiasa wanalijua hilo. Hivyo watu wachache kama wewe hawataweza kusikilizwa. Watu wamejigawa kimakundi kufuatana na itikadi bila kujua wanachofanya kutunisha mifuko ya wanasiasa na wanasiasa wanachofanya ni kutumia mianya hiyo ili kujinufaisha wenyewe, kufukuzana katika chama sababu ya kutofautiana ki mitizamo kwa kisingizio cha kuwa wasaliti.

Kuna Mbunge wa Conservative alihamia UKIP kwa kutokukubaliana na msimamamo wa chama chake lakini hajaitwa Msaliti wala hajatukanwa na wafuasi wa Conservative.

Zitto kakorofishana na uongozi wa CHADEMA kachambwa na viongozi wote wa CHADEMA mpaka kuitwa msaliti.

Lowasa kahama CCM kwa kutofautiana na uongozi wa chama chake, kaanza kushambuliwa na viongozi wenzake mpaka wafuasi wa ccm.

Lipumba alijiengua uongozi wa CUF kwasababu alizozijua mwenyewe bila kuhama chama lakini aliitwa Msaliti.

Sasa viongozi wa vyama vyote kikiwepo kinachoongoza kuua demokrasia cha CCM wanahubiri demokrasia. Mimi binafsi siijui demokrasia gani wanyoihubiri wakati wao wenyewe wanafeli katika mtihani wa demokrasia.

technically mimi na wewe hua tunatofautiana katika baadhi ya maeneo lakini hua hatutukanani sababu hii ni demokrasia lazima tukubali kutokukubaliana lakini kuna wanazi hapa wa CCM na CDM hilo halipo katika vocabulary yao na ndiyo wanasiasa kwa kupitia watu kama hao wanazidi ya kutupeleka hapa tulipo.

naomba maoni yako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…