Kwa yanayofanyika hii si ni sifa kwa wapinzani.

bendaki

JF-Expert Member
Feb 5, 2013
952
346
Wapinzani waliingia katika mpambano na chama tawala. Kazi ya wapinzani ilikuwa kila mpambano ulipokuwa ukijili wanaweka hadharani maovu yote yaliyokuwa yakifanywa na watawala na watenfaji wao. Na watawala wao kazi yao ilikuwa kukataa, kubeza na kutukana. Hata rais tuliyenaye alishiriki vilivyo akiwa upande wa watawala kwa kukataa, kubeza na kutukana.

Ili waweze kufanikisha walifanya mengi mabovu hayatasahaulika. Walituweka watanzania ktk matabaka. Mfano ni elimu. Walitengeneza mfumo wa Elimu unaozalisha wasomi wazuri wachache wakuja kuendelea kutawala. Mfumo wa Elimu huo kuzali watu wa kati wakuja kuwatumikia watawala. Lakini mfumo huo kubaza wengi wa Watanzania na Elimu duni ili wake kuwa wapagazi wa watawala na watendaji wao. Zilianzishwa shule za kata. Ilifutwa Elimu bure kwa vyuo na vyuo vikuu. Kukatungwa sheria gandamizi ya mkopo wa Elimu ya juu na vyuo ikilenga watoto wa makabwera kuwa vigumu kupata.

Huo ni mfano mmoja tu lakini mifano ni mingi ambayo Labda ipo na inalindwa na sheria zaidi ya 1000 zilizopitishwa kwa kauli za ipiteeee na ndiyoooo.
Wapinzani wakawa hawachoki kusema kila nafasi ilipopatikana lakini walikebehiwa sana sana na walipo jaribu kulazimusha kwa kutumia mbinu halalu kama maandamano nk walipigwa hata kuuwawa. Wananchi walilishwa sumu kwa propaganda kali zilizobebwa na nguvu za dola kama vile kufungia magazeti.

Ikafika sisi wananchi tukaanza kujitambua baada ya ufisadi, ubadhirifu, wizi wa Mali za umma, rushes na magendo kukiwemo kuingiza madawa ya kulevya vikiendelea as nobodies business. Kila shimo bovu na kila aliyekuwa mshiriki wa hayo mabovu alijulikana kwa viongozi, watawala, polisi, jeshi, Tiss na hata kwa baadhi ya watu wa kawaida. Yeyote ungemwambia nenda uwakamate ni kazi ndogo sana lakini kwa miongo kadhaa watawala walikataa kufanya hivyo.

Tulipo fika mwisho na Katibu na uchaguzi wananchi wakahamasishwa kuuondoa utawala uliokuwa umetufikisha Watanzania mahali pabaya. Watanzania wakadhamiria kuuondoa na kila mtawala akaliona hilo. Gadhabu ilikuwa na Labda bado ni kubwa. Hivyo kwa busara za kawaida MTU ni kuonyesha walio pandwa hasira kuwa umekuja kuwatumikia ili ghadhabu zao zishuke. Na inawezekana ukarudi ktk ranging yako baada ya gadhabu za watu kuteremka.

Katika mazingira hayo:
1. Kwa nini wapinzani wasifikiriwe kupewa pingezi kwa kuwa vishababishi wakupelekea watawala kusalimu amri?
2. Kwa nini ktk kunyosha mambo kusiende sambamba nabkufikiria kuwalipa Waathirika wa hali iliyifikiwa kwa kufikishwa hapo? Wananchi wamekosa Elimu, wamedhoofika afya zao, wamekosa maji, wamejuwa maskini na familia zao zimesambaratika nk nk. Natoa hoja wafidiwe!.
 
Tatizo la ccm ni ubinafsi na ushamba, wao wanafikiri ukiwa chama pinzani ni uadui ukipongeza jambo lililofanywa na mpinzani unaangamizwa.
 
Back
Top Bottom