Kwa yaliyotokea, ni wazi naanza kupata mental illness au effects za vitu nilivyotumia awali

Kuna vitu nimevifanya week hii vishaanza kunigharimu ninekosana na Kila mtu kuanzia wazazi mpaka ndugu na jamaa wananishauri nijirudi ila point niliyofikia nikisema nijirudi saikolojia yangu inaenda kuwa destroyed kabisa pengine naweza kuwa kichaa.

Week nzima nipo kwenye mabus nasafiri hata sijui naenda wapi nikifika destination akili inaniambia ondoka hapa hapakufai na pesa yote karibia naimalizia kwenye kusafiri mpaka Sasa sijui hatma ya niendako na kwenye kichwa changu Kuna fikra zinanijia kuwa naenda kuishiwa pesa ugenini kitu kitakachopelekea kuuza vitu vyangu nilivyonavyo kama simu na nguo then mapambano ndo yaanze sipendi kufika stage hiyo lakini naona inakuja.
Nenda lindi uje utupe mrejesho
 
Jtatu nilikuwa Dodoma nikaenda Iringa nikaona sio nikaenda Dar nimekaa masaa nikaenda kukata tiketi ya Njombe nikaona chenga nikaenda Makambako napo akili ikaniambie niende Mafinga napo nikaona chenga Sasa nipo kwenye bus naelekea Tunduru lengo ni hata mishe zikibuma nitembee hata Kwa miguu kijijini kwetu kwenda kufagilia makaburi ya wazee pengine mizimu imekasirika
Nitafute nikushauri
 
Nilifikia stage hii sema kuna sababu flani ilinizuia kuanza safari bila mpangilio...
Naomba sana Mungu aingilie kati nikae sawa
Pole Sana Binti najua msiba wa mama unekuathiri Sana .Karibu kuongea na watu ,kwa simu na hata ana kwa ana.
 
Dah,hivi inawezekana ukawa na stress kiasi Cha kufanya safari bila mpangilio kumbe
Ishanikutaga hii changamoto kubwa ilinikuta, ndugu na wazazi wakanikatisha tamaa kabisa niliondoka home kwa hasira na msongo nikawa Nasafiri naenda nisikokujua na nilisema nitakapoishia ndio hapohapo napiga kambi, nikiwa naelekea songea tukashuka Tunduru Bus Terminal kupata chakula na kujisaidia zile dk10, nilivyoshuka kwenye gari likanijia wazo lingine hapohapo nikapanda tena ndani kuchukua begi langu, nikiwa nawaza namna ya kwenda nchi jirani nikapiga kambi ya siku3 hapo Tunduru kupumzisha ubongo, nikapata wazo la kubaki hapo nikatafuta chumba nikaishi hapo kwa mwaka mmoja na miezi 3 ndipo nikarudi home nikiwa na ahueni ya stress na maisha yakaendelea, its now a different story.
 
Kuna vitu nimevifanya week hii vishaanza kunigharimu ninekosana na Kila mtu kuanzia wazazi mpaka ndugu na jamaa wananishauri nijirudi ila point niliyofikia nikisema nijirudi saikolojia yangu inaenda kuwa destroyed kabisa pengine naweza kuwa kichaa.

Week nzima nipo kwenye mabus nasafiri hata sijui naenda wapi nikifika destination akili inaniambia ondoka hapa hapakufai na pesa yote karibia naimalizia kwenye kusafiri mpaka Sasa sijui hatma ya niendako na kwenye kichwa changu Kuna fikra zinanijia kuwa naenda kuishiwa pesa ugenini kitu kitakachopelekea kuuza vitu vyangu nilivyonavyo kama simu na nguo then mapambano ndo yaanze sipendi kufika stage hiyo lakini naona inakuja.
Andika kwa kiingereza
 
Ishanikutaga hii changamoto kubwa ilinikuta, ndugu na wazazi wakanikatisha tamaa kabisa niliondoka home kwa hasira na msongo nikawa Nasafiri naenda nisikokujua na nilisema nitakapoishia ndio hapohapo napiga kambi, nikiwa naelekea songea tukashuka Tunduru Bus Terminal kupata chakula na kujisaidia zile dk10, nilivyoshuka kwenye gari likanijia wazo lingine hapohapo nikapanda tena ndani kuchukua begi langu, nikiwa nawaza namna ya kwenda nchi jirani nikapiga kambi ya siku3 hapo Tunduru kupumzisha ubongo, nikapata wazo la kubaki hapo nikatafuta chumba nikaishi hapo kwa mwaka mmoja na miezi 3 ndipo nikarudi home nikiwa na ahueni ya stress na maisha yakaendelea, its now a different story.
Duh,hila nikweli ukihama mazingira fulani, inasaidia kutuliza akili sometimes,
 
Back
Top Bottom