Kwa Wizi Huu: Jeshi lichukue uongozi wa Nchi

jojipoji koromije

JF-Expert Member
Mar 22, 2017
909
1,000
Inasikitisha sana, inauma sana ya kwamba watu tuliowaamini na chama tawala CCM kilichoaminiwa na wananchi kuwa kitatuongoza kutuletea maendeleo Kumbe ilikuwa ni unafiki na ulaghai wa hali ya juu. CCM pamoja na viongozi wake waandamizi mmegeuka na kuwa wanyonyaji, wezi wa mali zetu asilia sisi watanzani pamoja Na kizazi chetu kijacho Kwa manufaa yenu binafsi na familia zenu na wezi wenzenu!!!!! Manyang'au wakubwa nyie. Mkumbuke viongozi wote mnaohusika Na Wizi wa fedha Za dhahabu mmesomeshwa bure na Baba wa Taifa, Mzee Wetu Julius Kambarage Nyerere . Leo mmegeuka kuwa mafisadi wakubwa!! Hamna hata huruma na sisi watanzania wenzenu!!!! Mkasaini mikataba ya kinyonyaji ya raslimali zetu Kwa manufaa yenu binafsi!!!! Walahi mnastahili kunyongwa Mpaka Kufa hadharani.
Ili kuepukana na haya matatizo yanayoendelea kuletwa na CCM na viongozi wake napendekeza Jeshi La Wananchi wa Tanzania lichukue hatamu za uongozi wa nchi HARAKA SANA!!!! Na CCM ifutwe mara Moja kwenye vitabu na Ramani ya Nchi yetu pendwa ya Tanzania. Baba wa Taifa Mzee Julius Kambarage Nyerere alipoianzisha CCM, au alipopigania uhuru wa Nchi yetu hakumaanisha kuja kuwanyonya sisi wananchi wake bali kutuletea maendeleo ya kiuchumi kupitia raslimali tulizonazo. Sasa kwa ulaghai, ufedhuli, ufisadi na wizi huu Mkubwa uliofanywa na Viongozi waandamizi wa CCM Na serikali yake KUNA UHALALI GANI wa hiki chama na serikali yake kuendelea kuwa madarakani!!!!!????
Ni vizuri Jeshi la Wananchi lichukue uongozi wa Nchi Kwa muda wa miaka mitatu na ndani ya miaka hiyo mitatu ufanyike uundaji wa katiba mpya Kwa kuwashirikisha Wadau mbalimbali , kuwaondelea kinga ya kushitakiwa marais wastaaf, shughuli za kisiasa ziendelee lakini ziwe na mipaka, na hakutakuwa na uchaguzi wa Kitaifa Kwa muda wote huo labda kwa ngazi za vyama vya kisiasa, CCM ifutiliwe mbali lakini wapewe fursa ya kuunda chama kipya; na bunge livunjwe, Jeshi Kwa kushirikiana na watalaam lizipitie katiba za vyama ili zile ambazo zitakuwa si za kidemokrasia na zenye mlengo wa kinyonyaji zifutiliwe mbali na ikibidi kukifutia chama usajili, wahusika wote wa ufisadi wapelekwe mahakama za kijeshi ambako watashitakiwa na watakaobainika kuhusika uhujumu uchumi huu wa raslimali zetu wahukumiwe kunyongwa hadharani ili iwe fundisho kwa kizazi hiki na kijacho na pia jeshi lifutilie mbali mikataba yote ya uwekezaji katika sekta ya nishati na Madini ili tujipange upya!!!!
NASEMA HAYA KWASABABU LIBYA CHINI YA GADDAFI WALIFANYA HIVI NA WAKAFANIKIWA KULETA MAPINDUZI YA KIUCHUMI NCHINI MWAO.
Mwisho kabisa nampongeza Rais Magufuli kwa kuweza kutusaidia kutambua chama chake cha CCM Na serikali yake wanavyoneemeka na keki ya Taifa huku ikituacha wananchi tuliowengi tukibaki katika lindi kubwa la umaskini; huku wananchi wakiwa hawana madawa hospitalini, watoto wakikaa chini mashuleni huku wengine wakisomea chini ya miti!!!!! Wakulima hawana pembejeo!!! Kero lukuki!!!!
Lakini cha MUHIMU zaidi Rais hawezi kuepuka kutokuwemo kwenye uhujumu uchumi huu wa raslimali za Taifa kwani maamuzi mengi yalifanyika wakati na yeye akiwa ni sehemu ya wafanya maamuzi; na pia ana mikataba mingi ya gizani!!! Mfano ununuzi wa ndege!!! Ulipitishwa bunge gani? Au fedha zake zilipitishwa Na kikao cha bunge gani!!!!?? TUPO KWENYE MAJONZI MAKUU WATANZANIA!!!! Ndio Maana nasema ni HERI JESHI LA WANANCHI WA TANZANIA (JWTZ) LICHUKUE UONGOZI WA NCHI ILI TUEPUKANE NA UONGOZI HUU WA UFISADI, RUSHWA NA KINYONYAJI.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom