Kwa wamiliki wote wa magari ya Nissan tukutane hapa

Nataka kununua Nissan Datsun pickup single cab ....naomba ufahamu pipo..,
1569413550237.png
 
Aisee...pengine ana hela nyingi tu ila si mzoefu wa magari...ndiyo anaomba ushauri...maoni yangu.
:) ungemuacha tu ..sio kila mtu ni wa kumjibu kwenye hii mitandao...wengine ma prof, wengine ma zuzu.., wengine millionaires..wengine kabwela ., wakati mwingine unaweza kua unajibizana na mtu ambae ingekua ni face to face...huwezi hata kumgeukia kumuangalia.
 
:) ungemuacha tu ..sio kila mtu ni wa kumjibu kwenye hii mitandao...wengine ma prof, wengine ma zuzu.., wengine millionaires..wengine kabwela ., wakati mwingine unaweza kua unajibizana na mtu ambae ingekua ni face to face...huwezi hata kumgeukia kumuangalia.
Ni kweli kabsa...halafu watu wa namna hii hawajawahi kumiliki hata baiskel..
 
Mkuu mimi nimetumia za Nissan mbili, nilianza na Nissan cube, kagari kangu ka kwanza kabisa ka kuanzia maisha. Haka nilikaa nako miaka 5. Pamoja na udogo wake, kalikuwa very stable barabarani, kipindi cha kikombe cha babu kalitoka iringa hafi loliondo-samunge kwa babu na kurudi iringa. Mpaka nakauza, sikuwahi kupata changamoto kubwa zaidi ya zile za kawaida. Spear pia nilikuwa napata japo bei ilikuwa juu kidogo ukilinganisha na magari ya ukubwa huo ya kampuni ya Toyota. Hata hivyo, spear yake ilikuwa inadumu muda mrefu sana ikifungwa.

Baada ya hapo nikanunua Nissan Serena. Hii ngoma nayo iko vizuri sana. Very stable na inatumia umeme mwingi hivyo mafuta pia inakula kidogo. Injini zake ni sawa na Nissan xtrial. Zinachanganya haraka na zinakimbia sana. Very stable. Kwenye kosa utaifurahia, mwingine akiiga anapingua gari. Safari zangu nyingi ni barabara ya Iringa-mbeya.

Kona za iyovi sijawahi jutia kuwa na hii gari. Mara zote huwa natembea 120km/h na huwezi fikiri uko kwa Kona, very stable. Kwa Nissan Serena kidogo nmekutana na changamoto ya spear, kuna kipindi nimetafuta cv joint na sikupata inayoingiliana na gari yangu japo nilipata nyingi zinazofanana. Ika ibidi niagizie befoward wakaniletea. Nayo spear ukifunga unasahau.

Pia spear zake ziko juu kidogo, kwa mfano niliwahi kupasua Sterling power pipe, ilichukua 250,000 kupata ya kwake. Hii nmekaa nayo mwaka wa tatu na haijawahi nipa tabu kabisa.
 
Back
Top Bottom