Kwa waliosoma Dom miaka ya tisini

Kwa waliosoma Dom miaka ya tisini

chaArusha

Member
Joined
Mar 24, 2011
Posts
88
Reaction score
31
Shalom wakuu.
Na mimi leo nimeshawishika kukumbuka kidogo mambo ya zamani hasa wale waliokulia katika mji wa Dodoma kuanzia miaka ile ya themanini hadi tisini. Nakumbuka kipindi kile kulikuwa na ushindani mkubwa sana kwenye soka, hasa za sekondari. Kulikuwa na shule kama Dom Sec, Central, Jamhuri, Mazengo, Nzoisa na nyinginezo.
Lakini kulikuwa na ushindani mkubwa sana kwa shule za mjini. Kuna kipindi ilionekana kama Jamhuri ndiyo ili-dominate soka pale kwani ilikuwa tishio sana hadi katika fainali za mwaka 1989, nakumbuka baada ya kuwafunga Mazengo katika fainali na kuchukua taji la umiseta mkoa (nakumbuka ilikuwa ndiyo mara ya kwanza Mazengo kupoteza taji na sijui kama ilishajirudia) walifukuzwa wachezaji, walimu na mashabiki kutoka Mazengo hadi relini.
Dah, ulikuwa wakati mzuri sana, nakumbuka Jamhuri ilikuwa na wachezaji mahiri kama Twaha Mpemba, Teddy Mwaja, Mussa Kilunguya, Kessy, Selemani Taji, Lumuli, Kindamba na mshkaji mmoja hivi namkumbuka kwa jina moja la Kanali.
Pale Central nawakumbuka sana Kidesu Bingi (marehemu), Gwamaka na kule Dom Sec walikuwepo akina Majaliwa, Misanya Bingi (mdogo wake Kidesu), Jimmy na wengine kibao. Ilikuwa ikichezwa mechi na mojawapo ya hizi timu, hasa Jamhuri, ni big match. Nakumbuka pia wakati huo kulikuwa na matozi wengi sana Central maana ndiyo timu ya watoto wa kishua enzi hizo, namkumbuka mshkaji mmoja wa kuitwa Hashim Mbwilo, Hango na mdogo wake aliitwa Andrew, akina Hamad Mkamba.
Enzi hizo disco lilipigwa sana NK pale Jamatini chini ya DJ Kessy, kulikuwaga na jamaa mmoja hivi baunsa anaitwa Yusuf aliogopwa sana, sinema ilikuwa hapohapo na ukumbi mwingine ulikuwa kule Kuu striti wakati huo ni full muvi za kihindi na kizungu kidogo.
Katika soka, timu zilizotamba ni CDA, Waziri Mkuu, Kurugenzi, NBC na Mapinduzi FC iliyomilikiwa na CCM. Dah, inanikumbusha mbali sana.
Timu za uswahilini zilikuwa ni Dandee United na jamaa mmoja hivi wa kuitwa Makamba alikuwa ndo kama mwenye timu, ana mkono mbovu hivi lakini akisema kitu kila mtu anasikiliza, ilikuwa timu ya watoto wa mjini kati, pia kulikuwa na timu kutoka Chamwino, ikiitwa War Bus ilijaa wahuni balaa wa Chamwino na Gwasa (Chang'ombe), kuna timu nyingine ya uswazi pia kutoka Airport, ikiitwa African Fighters, na zingine kama Makole na Nsuzuni.
Karibu mwenye chochote aje tukumbushane!!
 
Bila shaka hivi sasa utakuwa mhenga

Post sent using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom