Kutokana na Serikali kuwadharau Walimu, Kila mwalimu ajiunge na sera inayoitwa FUKAMA yani FUNDISHA KULINGANA NA MALIPO, mda unaobaki kafanye shughuli zako.
watakazana wakati wana njaa??? matokeo ya kukazana kwao yataonekana baada ya muda gani?? Kwa nini sekta nyingine wakikohoa kidogo tu wanasikilizwa na sio waalimu????
uzalendo ndio utakalo liokoa taifa, ukishindwa kuwa mzalendo hata hao watoto unaowanyima haki yao ipo siku watakufungia darasani na kukutenda ambayo hutaamini waulize walimu wa kilwa na kibiti wakufahamishe matunda ya kutotimiza wajibu wao kama wazazi, walezi na walimu!wewe ndio unagundua sasa? mbona wenzako tunaitekeleza sera hii siku mingi? ndio maana hata mshahara ukiwa mdogo hatulalamiki kwani tunahakikisha tunatengeneza mshahara mwingine ili kwenda sammbamba na wenzetu wa kada zingine mambo ukiyapangilia utajikuta unamzidi hata BANK TELLER mwisho wa mwezi ila ukijifanya 'MZALENDO' kwenye nchi ya kifisadi utakufa siku sio zako!
Nakumbuka kauli alioitoa Edward Lowasa mwaka 1994 nikuwa chuo cha ualimu Monduli akimtetea mkuu wa chuo wakati huo (Def) Kuwa "if you are looking for the green pasture then you are in wrong way".Sakata lenyewe lilikuwa linahusiana na kula ugali mfululizo wakati fedha za kununulia mchele zikiwa zimefisadiwa.
Sasa hilo linadhihirika waalimu wakiwa wanataabika na familia zao,wanadharaulika na jamii ambayo wanatarajia watoto wao watafundishwa na walimu hao hao.
Na wasihi walimu wajiendeleze na fani zingine bila kusahau ujasiria mali ambao utawatoa kimaisha na waache kukopakopa ovyo kwenye vyombo vya fedha vya mafisadi kule unapokopa 1million na unalipa 4million.Na kule tunapoacha kadi za benki rehani.
Tuwasaidie watoto wa wakulima maana hao wanao tufanyia ufisadi watoto wao wanasoma shule za bei mbaya na pengine nje ya nchi,hivyo wanaweza wasiathirike na "FUKAMA" ikawa ni sawa na unajipiga na bastola kwenye mguu wako mwenyewe.
Tushirikiane kudai haki zetu kila moja kwa nafasi yake,wilayani ofisi za elimu ndo usiseme Mafisadi wa kutupwa,miungu watu,wana wahujumu walimu wenzao.
Wakaguzi hawapendi kucheza game maofisini,Hawatengewi fedha za kutosha kukagua,magari yao hayana mafuta,mpaka wakajipendekeze kwa wakurugenzi,unatarajia watakagua?kuna walimu feki wengi kwenye private schools,wageni toka nchi jirani mradi anaongea kiingereza anaajiriwa."tatizo ni kwamba wakaguzi wa shule wanakula viyoyozi maofisini lakini laiti wangekuwa wanapita kwenye shule za kata maarufa kama "saint kayumba" wasinge rudia tena kucheza game maofisini maana hali ni mbaya" na mbaya zaidi wanaoumia ni watoto wa mkulima kama mimi" walimu baada ya kutishiwa wakitaka kuandamana kudai stahiki zao,sasa kila mmoja ameamua kugoma kwa style anayoweza wengine wanaishia bustanini,wengine kwenye mazizi ya ng'ombe,na wengine wanaumwa mafua miezi mitatu,sijui miaka ishirini ijayo tutavuna kizazi cha aina gani kama si majambazi wasomi"
Kama haki inadiwa na haipatikani tufanyaje?