Kwa walichokifanya Mbagala leo, Polisi sasa wanatia aibu

Hivi juzi lile tangazo la kujiunga na jeshi la polisi lilisema kigezo cha kujiunga na jeshi hilo mtu awe Division ngapi kwny matokeo yake ya form 4/6?
 
Polisi Sasa wanatenda haki kila Kona, Kama sio msimbazi Ni Mara na leo Mbagala.
 
Pale mbagala kizuiani kuna mgomo wa wafanyakazi wa kampuni ya sino hydro, wanaojenga barabara ya mwendokasi ya kilwa load. Wana siku ya tatu wakigoma kushinikiza madai yao.

Ila asubuhi ya leo walifika polisi wakiwa na silaha,bila kuuza chochote kutoka kwa wafanyakazi wakaanza kuwavulumishia mabomu ya machozi.Katika hali ya kushangaza hakuna hata mfanyakazi mmoja aliyekimbia badala yake walikaa chini. Mabomu yaliendelea hata baada ya watu kukaa chini. Hakukimbia mtu .

Watu wanateseka kwa moshi mzito wa mabomu, polisi wakawa wanacheka huku wafanyakazi wale wanyonge wakiinamisha vichwa vyao chini kukwepa moshi.

Askari wetu badilikeni
RIP Hamza
 
Askari wenye uwezo wa kureason ni wachache sana, mostly wanaamini nguvu ndo kila kitu kwao.
Polisi hawatakiwi kutumia akili ni kufuata maagizo wanayopewa tu,kama mnyama uliyemfuga kwa ulinzi akianza kugomea maagizo yako hafai ni wa kumpoteza.
Hapo ni kujiuliza waliotoa maagizo
 
Kama walionyesha utulivu hakukuwa na haja ya kupigwa mabom.. Watu wakireact wataambiwa Ni Wafia.....
...eti jaman, unapigaje mabomu watu ambao hawana silaha, hawajafanya fujo wala vurugu yoyote? Very pathetic....😳😳😳
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Inasikitisha sana watu wanadai haki zao ndani ya nchi yao wanayodhulumiwa nadhani hiyo kampuni ni ya Wachina wanaishia kupigwa mabomu na kukamatwa!!!
Pale mbagala kizuiani kuna mgomo wa wafanyakazi wa kampuni ya sino hydro, wanaojenga barabara ya mwendokasi ya kilwa load. Wana siku ya tatu wakigoma kushinikiza madai yao.

Ila asubuhi ya leo walifika polisi wakiwa na silaha,bila kuuza chochote kutoka kwa wafanyakazi wakaanza kuwavulumishia mabomu ya machozi.Katika hali ya kushangaza hakuna hata mfanyakazi mmoja aliyekimbia badala yake walikaa chini. Mabomu yaliendelea hata baada ya watu kukaa chini. Hakukimbia mtu .

Watu wanateseka kwa moshi mzito wa mabomu, polisi wakawa wanacheka huku wafanyakazi wale wanyonge wakiinamisha vichwa vyao chini kukwepa moshi.

Askari wetu badilikeni
 
Screenshot_20210905-210652~2.jpg
 
Sidhani kama polisi wanapewa mafunzo ya kutosha jinsi ya kulinda usalama wa raia, na kuna tatizo katika kutambuwa nani awe polisi au nani hafai, na sidhani kama wanajuwa jukumu lao namba moja ni KULINDA USALAMA WA RAIA, siyo kiwanyima haki, kuwanyanyasa, kuwatisha au kuwatesa, lazima wakemewe mpaka wajuwe, Afande Kandaga yuko wapi?!
 
Back
Top Bottom