Synthesizer
Platinum Member
- Feb 15, 2010
- 12,272
- 21,448
Nimetafakari sana kwa nini inakuwa ngumu sana kwa vyama vya upinzani kuiondoa CCM madarakani. Achana na shutuma kwamba CCM wanaiba kura, ambazo zinaweza kuwa kweli au uongo. Kosa kubwa sana vyama vya upinzani wanafanya ni kutozingatia mambo mawili;
1. CCM ni lichama kubwa lenye nguvu
2. Wapiga kura wengi wa Tanzania ni wenye ufahamu mdogo sana wa utawala bora.
Ushauri wangu kwa vyama vya upinzani ni kwamba;
1. Kukabiliana na lichama kubwa na lenye nguvu kama CCM tumia filosofia ya "kama wewe ni mti mkubwa sie tutakuwa shoka dogo lililonolewa kukukata na kukuangusha". Huwezi kukabiliana na CCM kwa kutumia nguvu hata siku moja (confrontational approach) - mambo ya kura ya kukosa imani na raisi, kumgomea naibu speaker, maandamano nchi nzima nk hayatakusaidia - ni sawa na kutaka kuuangusha mti mkubwa kwa kuusukuma. Inapobidi, ili kuwa shoka kali, kubaliana na CCM mambo kadhaa yanayogusa watu na yafanyie kazi hata zaidi. Na by the way, kama chama kimoja kimoja cha upinzani hamuwezi kamwe kuusukuma mti wa CCM hadi ukaanguka. Sahau.
2. Badilisha aina ya ujumbe kulingana na mazingira. Ni wapiga kura wachache sana wanauelewa ujumbe wa Eskrow, Richmond nk. Ni muhimu sana ukumbuke Watanzania wengi wanaouelewa ujumbe wa vyama vya upinzani juu ya mambo mbalimbali hawajitokezi kupiga kura. Badilisha approach - usigangamale kwenye ujumbe tu.