Kwa vyama hivi CCM, CHADEMA, CUF,TLP......

Mihayo

JF-Expert Member
Apr 12, 2010
268
62
Nimekuwa nikifatilia kwa makini mwenendo wa kisiasa katika nchi yetu kwa zaidi ya miaka 20 sasa. Nasikiitika kusema sioni chama makini wala chenye dhamira ya kweli kuwaongoza Watanzania kwenda kwenye nchi ya asali na Maziwa... Kama kipo basi sera na madhumuni yake yanaweza kuwa sahihi laikini hakina watu sahihi!!! Kizazi hiki kilicho pata bahati ya kulelewa na waasisi wa nchi kimegeuka na kuwa kituko ama kwa makusudi au kwa kujua, Mbaya zaidi kinahakikisha hakitoki madarakani iwe ndani ya chama au kwenye uongozi wa kiserekali. Namkumbuka mwalimu wangu wa Siasa siku hizo na naamini ni wakati sahihi sisi tulioamua kuwaachia hawa wanaojiita wanasiasa na tuliowamini wanaweza kutuongoza kuamuka na kuunganisha nguvu tuwapinge kwa hoja na tuwe na chama sahihi si kwa masilahi yetu binafsi bali kwa manufaa ya nchi yetu na vizazi vijavyo. Najua wengi tumejenga huruka ya uoga, Najaribu kujiuliza wale wazalendo tuliokuwa pale Mlimani miaka ya 90's na kurudi nyuma kidogo tunashindwa nini kuwaunganisha vijana wetu ili kuwa na chama sahihi.
Kama tuliweza kusimama kutetea masilahi ya nchi wakati ule sasa tumekuwa nini???? Nasikia sisi ndo ambao hatutaki wanetu wapate shida wakati sisi tulisoma kwa shida na uzalendo wa hali ya juu kwa nchi yetu. Wazalendo Tuamuke nchi hii ni yetu CCM, CHADEMA, CUF..... Hawana dhamira ya kweli kutupeleka tunakota. Nimechokoza
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom