Gangongine
JF-Expert Member
- Dec 31, 2015
- 3,854
- 1,776
Inashangaza Siasa za Upinzani zimekuwa kituko kwa kukosa Ajenda za Msingi zinazobeba matatizo ya wananchi.
Badala ya kuongelea mambo ya msingi kama elimu, maji, afya, ushirika, uchumi nk kwa kutoa suluhisho au Sera mbadala, Wapinzani inaonekana hawana haja ya kuchukua dola kabisa kwa kuacha ajenda za Msingi na kufanya Siasa za Kisanii kama kutumia majanga kama ajenda yao Kisiasa.
Mfano ni hivi sasa ambapo uhaba wa Chakula unatumiwa kama kete ya Kisiasa kwa baadhi ya Wapinzani. Cha kujiuliza ni kwamba ikiwa wao watakwenda Ikulu (2055) haya majanga hayatatokea?
Pili ni unafiki wa Wapinzani kuwadanganya Wananchi kwamba Serikali ina wajibu wa kuwajengea nyumba wananchi wakati hakuna Serikali yoyote duniani iliyowahi kufanya hivyo zaidi ya kutoa msaada wa dharura wa chakula na mahema mpaka pale ambapo wananchi watapata uwezo wa kurekebisha makazi yao. Inasikitisha kwa Chama cha Upinzani kudhani kwamba kuchochea chuki baina ya Serikali na wananchi ndio iwe njia ya kwenda Ikulu. Huu si ukomavu wa Kisiasa hata kidogo.
Tatu inasikitisha pia kuona Wapinzani hao hao waliomuita Rais Mstaafu JK kuwa ni Dhaifu, wamegeuka na kulaumu kwamba tuna Utawala wa Kidikteta. Kwa unafiki wao wanaanza kudai wame 'miss' utawala wa JK. Ukichunguza kwa undani kumbe walifurahia kwenda Ikulu kunywa Juice jambo ambalo siku hizi halipo.
Kama kweli wanataka kwenda Ikulu mapema kabla ya 2055 basi inabidi watueleze watakachofanya tofauti na kinachofanywa na Chama Tawala ni kipi na Fedha za kufanywa hayo watazitoa wapi. Bila Sera Mbadala, watabaki kuchochea vurugu na kuandamana miaka yote bila kushika Dola!