Kwa uhai wa CHADEMA lazima M/kiti wa Mbowe kuvuliwa uwenyekiti wa chama

josegorofani

Senior Member
Aug 19, 2015
197
69
Katika hali isiyo ya kawaida Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) kimejivuruga katika kupambana na Paul Makonda baaada ya kumtaja M/Kiti Mbowe kujihusisha na Dawa za Kulevya hivyo kupoteza Dira na Malengo ya Chama hiko. Chadema nimekuwa Chama kikuu cha upinzania Tanzania lakini kwa hali hii kinazidi kushuka mpaka level ya kupambana na RC! Nashindwa kuelewa ni nani aliyewaroga!? na hiko wapi Dhamira, Dira, Ilani au mlengo wao katika Siasa za Tanzania.

Kukamatwa kwa Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe dhidi ya kujihusisha na dawa za kulevya imekuwa pigo kubwa kwa Chadema A na Chadema B(ACT) na kuwapeleke kushuka katika Siasa, katika kipindi hiki mnapaswa kujitafakari na ikiwezekana kumvua Uenyekiti Mbowe kwakuwa amekidhalilisha Chama na Kiti, pia kuwaingiza katika kashfa nzito ya Dawa za Kulevya jambo ambalo linawapotezea uaminifu kwa wananchi.

Ushauri; CHADEMA MVUENI UENYEKITI MBOWE ILI CHADEMA IWE SALAMA NA KUJISAFISHA KATIKA SUALA HILI LA MADAWA YA KULEVYWA

Mbowe.jpg
 
Sawa tumekuelewa lakini kwanza tunaomba index namba ya Makonda (Daudi Christian Bashite) ya mitihani yake ya O-level na A-level! Ukiweza tupe na majina kamili ya wazazi wake!
Mfuate ofisini kwake atakupatia ufafanuzi Ila hapa nashauri huyu Mwenyekiti wa kudumu avuliwe uongozi wake maana ameshajiusisha na Madawa ya Kulevya toka enzi zake za UDJ.
 
Mshaona 2020 sio mbali na hakuna lolote la maana mlilofanya ,sasa njia pekee nikuvivuruga vyama pinzani
Hilo mtashindwa kama ambavyo mmeshindwa kila kitu mpaka sasa
 
Mfuate ofisini kwake atakupatia ufafanuzi Ila hapa nashauri huyu Mwenyekiti wa kudumu avuliwe uongozi wake maana ameshajiusisha na Madawa ya Kulevya toka enzi zake za UDJ.
Acha maneno Daudi Christian Bashite, lete vyeti! Sisi hatuna shida na Mbowe, hajafoji vyeti mwenyekiti wetu.Tunasubiri serikali yenu ithibitishe kuwa anajihusisha na madawa ya kulevya ndio tumbadilishe!
 
MACCM mnamhofia sana huyu bingwa, mpaka mnaanza kutumia silaha za maangamizi, shame.
Hakuna hofu na M/Kiti wa kudumu ila lazima tunaona tunakosa wapinzani kutoa ushauri ili waamke na kuleta mshindani nasi tupate mshindani, maana kwa hii kwa sasa Tanzania hakuna mpinzani wa chama cha mapinduzi
 
Katika hali isiyo ya kawaida Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) kimejivuruga katika kupambana na Paul Makonda baaada ya kumtaja M/Kiti Mbowe kujihusisha na Dawa za Kulevya hivyo kupoteza Dira na Malengo ya Chama hiko. Chadema nimekuwa Chama kikuu cha upinzania Tanzania lakini kwa hali hii kinazidi kushuka mpaka level ya kupambana na RC! Nashindwa kuelewa ni nani aliyewaroga!? na hiko wapi Dhamira, Dira, Ilani au mlengo wao katika Siasa za Tanzania.

Kukamatwa kwa Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe dhidi ya kujihusisha na dawa za kulevya imekuwa pigo kubwa kwa Chadema A na Chadema B(ACT) na kuwapeleke kushuka katika Siasa, katika kipindi hiki mnapaswa kujitafakari na ikiwezekana kumvua Uenyekiti Mbowe kwakuwa amekidhalilisha Chama na Kiti, pia kuwaingiza katika kashfa nzito ya Dawa za Kulevya jambo ambalo linawapotezea uaminifu kwa wananchi.

Ushauri; CHADEMA MVUENI UENYEKITI MBOWE ILI CHADEMA IWE SALAMA NA KUJISAFISHA KATIKA SUALA HILI LA MADAWA YA KULEVYWA

Msiende Mwendokasi wakati hamna break.Mwambie Mwenyekiti wako ajiuzulu kwanza maana anavunja Katiba aliyoapa kuilinda.

Safari lazima muimbe tu.
 
Back
Top Bottom