Mmanu
JF-Expert Member
- Feb 11, 2015
- 1,745
- 987
Habari za sasa wakuu
Nakumbuka wakati wa utawala wa mh. Jk wa awamu ya nne wananchi wengi walisikika wakitoa malalamiko kwenda kwa rais yaliyohusu suala la kusafiri sana nchi za nje kuliko kudumu ndani. Hata ikulu ilipokuja kutoa utetezi kuwa anapita akiomba misaada mbalimbali kwa ajili ya miradi ya maendeleo na sekta mbalimbali ziweze kuhudumu bado alionekana hana maana kwa utetezi ule huku wakitoa hoja ya kuwa nchi inaweza kujitegemea kwa rasilimali zake zilizopo.
Hao hao baada ya MCC na wahisani wengine kutoka EU kujitoa wanakuja na nyingine ya kuilaumu serikali kwanini wasababishe kuukosa msaada MCC huku wakisahau hoja za mwanzo kuwa nchi ina rasilimali za kutosha kuweza kujitegemea.
Je ni kusema tunasahau tunachokisimamia?
Na kama taifa linaundwa na watu waliojawa na fikra za utegemimezi hili taifa litaweza kweli kujitemea?
Nawasilisha!