Kwa nini Wazungu(EUROPE) na US waizingire kijeshi Russia na Sio CHINA?

mitale na midimu

JF-Expert Member
Aug 26, 2015
10,420
17,728
Ni miaka sasa majeshi karibu yote ya ulaya yameweka kambi karibu na russia.
Kila siku mazoezi ya kivita makali yanaendelea karibu na mipaka ya Russia.
Upande wa Alaska marekani kaweka mitambo mikali ya kujizatiti
Marekani wamejaza mitambo ya kuzuia makombora ya Russia Ulaya.

Swali. Kwa nini Russia na Sio china?
China wako vizuri pia kiuchumi kitu ambacho kinaweza kuwafanya wakawa imara sana kijeshi pia maana watakuwa na pesa nyingi za kutengeneza silaha pia kuliko russia.

karibuni wajuzi wa mambo...

Picha:
592d3b71c36188f07e8b458b.jpg

Wanajeshi wa Marekani wakifanya mazoezi karibu na mpaka wa RUSSIA
nato-europe-drills-russia.jpg

Wanajeshi wa NATO ktk mazoezi karibu na Mpaka wa russia
56bc1f26c36188cd5c8b460f.jpg

Katika mazoezi
1020040206.jpg

Msafara wa magari ya kijeshi ya nNATO kuelekea karibu na mpaka wa RUSSIA.
US-troops-en-route-to-NATO-drills-in-Lithuania-Latvia-and-Estonia.jpg

Wanajeshi wa US wakiwa katika harakati zao karibu na russia.
f-natodrill-a-20160609.jpg

Zoezi kubwa la kijeshi la NATO lililofanyika poland katika harakati za pamoja kutaka kutia vitisho Russia.
 
nadhani historia ya kuenea kwa ujamaa
masuala ya kiusalama hasa kukuza eneo lake la kiushawishi eneo la mashariki ya Ulaya mfano Turkey nk
Teknolojia ya kijeshi hawa watu wamekua wanashindana hasa kwenye mambo ya nyuklia mfano vita baridi

kwa mawazo yangu bado China hajawa itisho sana kwa EU na NATO kwa maana wanamuona China yupo kiuchumi zaidi yaani anakimbia kukuza uchumi wake kidunia tofauti na ndugu yake Russia
Pili China imetoka kwa Muingereza miaka ya 1940s wakati huo tayari Russia yupo na mapambano na nchi za Ulaya Magharibi
 
Hao walojivika sijui ni mitambala sijui nyasi kichwani nao ni wanajeshi wa Ulaya hao? Hizo si ni mbinu enzi wa jeshi la kamanda Mkuu Chief Mkwawa?

Wangefanya JWTZ wetu comment za ajabu sana zingetoka hapa.
hao inaonekana wako tayari pia kwa guerrilla war. Maana lazima ikitokea wanapigana vita vya msituni haepukiki kwa russia.
Au mkuu kwa sababu tumezoea vita vya mwarabu kwenye michanga...
 
hakuna siku Marekani au nchi yeyote ya Ulaya itdhubutu kupigana vita na Russia. Maana kwanza ana Nuclear boombs nyingi kuliko nchi yeyote duniani na anazo BULAVA Father of all Bombs can wipe France kwa kombora moja tu.

hivi nadhani ni precautionary measures lakini vita kamili haitokaa itokee.
 
hao inaonekana wako tayari pia kwa guerrilla war. Maana lazima ikitokea wanapigana vita vya msituni haepukiki kwa russia.
Au mkuu kwa sababu tumezoea vita vya mwarabu kwenye michanga...
Nilikuwa nawatupia ujumbe wale waliokuwa wakibeza lile tizi la makomandoo wetu wa sangasanga, wakidai dunia iko kiteknolojia zaidi, hakuna kupasua matofali.
 
China anazingirwa na EU na USA kwenye maswala ya kiuchumi hasa biashara kwasababu china ni tishio kiuchumi lakini kijeshi Russia wako mbali sana kijeshi na kitecnolojia tofauti na china..

Vile vile inadaiwa eti urusi ana mpango wa siri wa kuimega kidogo kidogo ulaya kimabavu ile crimea ilikuwa ni mwanzo tu.

Yaani putin anataka kuirudisha USSR hata kwa ubabe...
Hii ndiyo mission yake nazan hata Ukraine Yale majimbo yanayoendelea kuleta utata kujitenga na Ukraine . hawa Russia wana influence yao.

Ndiyo raisi ya kuwa na Raisi ambaye amewahi kuwa usalama wa Taifa like ex KGB boss Putin . jamaa ni mzalendo na taifa lake na ni moja kati ya viongoz waliumia sana kuona USSR ikisambalatika
 
hakuna siku Marekani au nchi yeyote ya Ulaya itdhubutu kupigana vita na Russia. Maana kwanza ana Nuclear boombs nyingi kuliko nchi yeyote duniani na anazo BULAVA Father of all Bombs can wipe France kwa kombora moja tu.

hivi nadhani ni precautionary measures lakini vita kamili haitokaa itokee.
Uache uongo hata nuclear yenyewe haiwezi kuwipe out France yote kwa bomu moja
 
Hao walojivika sijui ni mitambala sijui nyasi kichwani nao ni wanajeshi wa Ulaya hao? Hizo si ni mbinu enzi wa jeshi la kamanda Mkuu Chief Mkwawa?

Wangefanya JWTZ wetu comment za ajabu sana zingetoka hapa.
Angalia tena hicho picha.. unaharaka gani?? we unadhani majani hayo..?? Ni nguo hiyo mahsusi kwa ajili ya msituni..
 
Kwa wana theologia ya vita na milango ya kuzimu ni kwamba milango ya kuelekea mwisho wa dunia utaanzia syria na utaenda afaghstan mpaka urusi,
sasa marekan wanafuata maagizo ya hao freemanson waliyoyatabiri ili neno litimie"VITA KUBWA DUNIANI".NA HUO NDIO UTAKUWA MWISHO WA DUNIA.
Ingawa kuna suala la nishati ya gesi,urusi akiikata gesi yake ulaya kwa asilimia kubwa itaathirika sana kwa kuwa humtegemea yeye sasa mawazo yangu USA anataka iwe kama uarabuni viwe chini ya maamuzi yake hata kama nchi nyingi zitashiriki vita.
MAWAZO YANGU NIKIWA KAMA MWANA JF.
 
Back
Top Bottom