Kwa nini wasomi wasikomboe taifa hili?

Kwa nini wasomi wasikomboe taifa hili?

Hosea Ben

Member
Joined
Sep 22, 2014
Posts
69
Reaction score
15
Humphrey Polepole Evarist Chahali Kitila Mkumbo na wanafiki wengine wote ni kweli mumefilisika kifikra hivyo? Juzi tu Chahali ulikuwa unabwata ati ccm wanakufuatilia ili wakuue, leo umekuwa kibaraka wao? Pia Polepole ulikuwa ulilia katiba ya Warioba ya serikali tatu ambayo ccm unayoitetea imeitupilia mbali, Ukawa wamechukua jukumu la umma kupata katika mpya, leo mnawapinga wananchi?
Utafiti unaonyesha kuwa tanzania ina idadi ya wajinga wengi wanaomiliki phd kuliko wajinga wanaolima kwa jembe la mkono kule vijijini,
Mchango wa wasomi wengi wenye hadhi ya u-professor katika kulijenga taifa ni sifuri kabisa, ila mchango wao katika kulidumaza taifa ni 100%.
Watu wa aina ya Lipumba, Kitila mukumbo, Zitto kabwe, Dr Bendon Bana ni sehemu ya gharika la taifa hili. Hawa wanayatazama ukubwa wa matumbo yao kuliko mstakabali wa taifa hili.
 
Njaa inatisha kuliko mlipuko wa ajali ya ndege....njaa inambadili msomi kuwa mjinga baba, au umesahau? Wacha nirudi kwenye mada......
Wasomi si tatizo katika nchi hii bali ni tabia ya wa TZ kupenda maisha ya bila kufanya kazi.....wasomi wetu wametumia fursa hiyo ili kupata maisha. Kwa bla bla tu anayopiga msomi inamwezesha kuishi miaka 20 bila kutegemea mshahara. Na bla bla hiyo ni kama vile kukaa kwenye kipindi cha TV na kuendesha mafmada ya kukua kwa uchumi ama kujadili umaskini jinsi ulivyopungua wakati akijua kabisa hicho anachokisema ni uongo! Lakini hoja yake si kile anachokisema kwenye kipindi bali ni kile atakachokipata baada ya kipindi.......! Yaani "fursa" ya kujipatia kipato kisicho halali ama kipato kwa njia ya bila kutoa jasho ndio imeifikisha nchi yetu hapa ilipo kupitia wasomi.....
 
Ni masikitiko makubwa,kwa hili Tanzania tutakua wasindikizaji wa maendeleo
 
Mkuu umeleta hoja nzuri kwa wakati muafaka!,Kiukweli Wasomi wa TZ ni hakunaga wao wanapenda kutetea Uongo mchana kweupe ili mradi tu mkono uende kinywani,Mimi ninathibutu kusema,Wasomi wetu wana Akili km za kuku,maana kuku hufikiri juu ya leo tu,yeye hana hbr na kesho.
 
Siku moja alikuwa anaongea professor bungeni. Maneno yake yalikuwa ni kurudia ya waliopita wote. Yaani hayana new value. Akaja mbunge wa meatu akaongea madini. Akaweka mawazo yake. Ubunifu na jinsi ya kuongezea halmashauri kipato. Nilichukia saana huu uprof amybao hauna value kwa locals. Nimeamua kuwa self made professor kwa kuinvest ktk kujidsomea na kuimpliment kila actionabe ideas.

Wasomi mbadilike. Mnajidharirisha
 
Humphrey Polepole Evarist Chahali Kitila Mkumbo na wanafiki wengine wote ni kweli mumefilisika kifikra hivyo? Juzi tu Chahali ulikuwa unabwata ati ccm wanakufuatilia ili wakuue, leo umekuwa kibaraka wao? Pia Polepole ulikuwa ulilia katiba ya Warioba ya serikali tatu ambayo ccm unayoitetea imeitupilia mbali, Ukawa wamechukua jukumu la umma kupata katika mpya, leo mnawapinga wananchi?
Utafiti unaonyesha kuwa tanzania ina idadi ya wajinga wengi wanaomiliki phd kuliko wajinga wanaolima kwa jembe la mkono kule vijijini,
Mchango wa wasomi wengi wenye hadhi ya u-professor katika kulijenga taifa ni sifuri kabisa, ila mchango wao katika kulidumaza taifa ni 100%.
Watu wa aina ya Lipumba, Kitila mukumbo, Zitto kabwe, Dr Bendon Bana ni sehemu ya gharika la taifa hili. Hawa wanayatazama ukubwa wa matumbo yao kuliko mstakabali wa taifa hili.

Hawaezi kulikomboa kwa sababu ya mfumo uliopo madarakani ni kuhakikisha taifa halikomboki ila wachache wenyemadaraka wanakomboka! msomi yeyote anaejitokeza kufanya kazi ya masilahi kwa taiga anatengenezewa zengwe watafanyaje ili maisha aende wanaulizwa wanachotaka nini wanajazwa mapesa kimya ukimwuliza 2x3 anakwambia 2 au 8 sababu kibao na watanzania waliowengi kwa sababu wamepumbazwa kwa wali, fulana, kanga, kofia n.k wanakubali. usione ajabu hata polepole labda keshatumiwa ujumbe mzito afanyeje!!! trh 25 mwisho wa hadithi hii. wasomi warudi kwenye taaluma akituletea hadithi za abunwasi anyongwe uwanja wa taifa SAA 6.00 mchana wenzake waone!!!
 
Back
Top Bottom