Napenda kuwasalimu wote mliopo kwenye jamiiforum kwani ni mara yangu ya kwanza kupost topic. Kuna jambo nisilolielewa labda mnaweza kunisaidia. Nimekuwa nikitafuta kazi kwa muda sasa japo nimejishikiza sehemu lakini bado sijatulia. Kinachonishangaza ni kwamba nimeenda kwenye interview kadhaa nafanya vizuri lakini mwisho wa siku unaambiwa "tukikuajiri tutakulipa nini?" Hapo hujaambiwa mshahara ni shilingi ngapi , hujaulizwa kama unakubaliana nao au la. Ninachojua unapaswa kuulizwa unataka shilingi ngapi halafu wao wanakwambia ngapi wanaweza kukulipa. Swala hili linanikwaza sana kwani sina elimu ya kutisha. Je ni njia tu ya kuninyima kazi? hebu nisaidieni wana jamii labda mimi ndio sielewi. Mwisho nawatakieni wote mwaka mpya mwema.