kwa nini unakosa ajira kwa watu kujiuliza tutakulipa nini? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

kwa nini unakosa ajira kwa watu kujiuliza tutakulipa nini?

Discussion in 'Nafasi za Kazi na Tenda' started by jakisek, Dec 30, 2011.

 1. j

  jakisek New Member

  #1
  Dec 30, 2011
  Joined: Dec 29, 2011
  Messages: 3
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Napenda kuwasalimu wote mliopo kwenye jamiiforum kwani ni mara yangu ya kwanza kupost topic. Kuna jambo nisilolielewa labda mnaweza kunisaidia. Nimekuwa nikitafuta kazi kwa muda sasa japo nimejishikiza sehemu lakini bado sijatulia. Kinachonishangaza ni kwamba nimeenda kwenye interview kadhaa nafanya vizuri lakini mwisho wa siku unaambiwa "tukikuajiri tutakulipa nini?" Hapo hujaambiwa mshahara ni shilingi ngapi , hujaulizwa kama unakubaliana nao au la. Ninachojua unapaswa kuulizwa unataka shilingi ngapi halafu wao wanakwambia ngapi wanaweza kukulipa. Swala hili linanikwaza sana kwani sina elimu ya kutisha. Je ni njia tu ya kuninyima kazi? hebu nisaidieni wana jamii labda mimi ndio sielewi. Mwisho nawatakieni wote mwaka mpya mwema.
   
 2. K

  Kubingwa JF-Expert Member

  #2
  Dec 30, 2011
  Joined: Apr 23, 2010
  Messages: 502
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Kama hawana cha kukulipa kwa nini wakuite kwenye interview?
   
 3. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #3
  Dec 30, 2011
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Hilo swali linaashiria ulitakiwa kuzunguka mbuyu..................aka kutoa mlungula!
   
 4. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #4
  Dec 30, 2011
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Hapana mkuu, nadhani ume'overlook.
   
 5. Mohamedi Mtoi

  Mohamedi Mtoi R I P

  #5
  Dec 30, 2011
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 3,326
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 0
  Siku nyingine ukiulizwa swali hilo waambie nataka niwe nalipwa fedha halali kwa malipo na kazi halali nitakayopewa na kutimiza wajibu wangu.
   
 6. Kalunguine

  Kalunguine JF-Expert Member

  #6
  Dec 30, 2011
  Joined: Jul 27, 2010
  Messages: 2,544
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Achana nao,tena wala isikuumize kichwa.Hao ni waajiri uchwara tu.Kwani ilikuwaje mpk wakakuita kwa interview?Just stay focused kuwa unatafuta kazi,ipo siku tu utakutana na mwajiri wa maana na sio hao wababaishaji wasiojielewa!Eeti tutakulipa nini?Kwani wao wanalipwa nini?wao pia si ni waajiriwa wa kampuni hiyo?
   
Loading...