Kwa nini tunasema mtu huyu AULA?

Kwa nini tunasema mtu huyu AULA?

Joined
Jul 23, 2010
Posts
44
Reaction score
15
Kwanini mtu anapoteuliwa ktk nafasi yoyote ya juu tunasema AMEULA? Wakati pale anakwenda kutumikia taifa ama shirika lolote ndani ama nje ya nchi, hatuoni kusema hivyo ni kuchochea RUSHWA, na UFISADI ktk nafasi hiyo kwa maana anakwenda KULA (Kuiba)?
 
Kwa Tanzania madaraka ni ulaji. Hakuna mbinyo wa kutosha kuwafanya wanaogombea madaraka kuona wanagombea kitu kigumu sana na chenye dhamana.

Kwa Tanzania kuwa kiongozi ndio mwisho wa umaskini na hakuna kuhojiwa au kuwajibika kikamilifu kutokana na makosa.

Ukiwa kiongozi Tanzania unaweza kufanya ujinga na ukakubalika tu

Hadi watu watakapotokwa na ujinga ndio dhana hii itabadilika

Lakini hadi wakati huo tutaona vita kati ya wale wanaowania urais kwani kwa mtazamo wao urais ni kazi rahisi na itawawezesha kufanya yote wayatakayo

Hapa Tanzania ni rahisi kuwa rais kuliko kuwa mkurugenzi wa kampuni binafsi

Kwanini mtu anapoteuliwa ktk nafasi yoyote ya juu tunasema AMEULA? Wakati pale anakwenda kutumikia taifa ama shirika lolote ndani ama nje ya nchi, hatuoni kusema hivyo ni kuchochea RUSHWA, na UFISADI ktk nafasi hiyo kwa maana anakwenda KULA (Kuiba)?

Kwa mfano njaa aliyokuwa nayo NAPE wakati ule hadi akakimbilia CCJ,na wakati huu kama Katibu mwenezi wa magamba,hauoni kama ameula?
 
Back
Top Bottom