kuamini wanasiasa ndicho chanzo cha umaskini wa watanzania.badala ya kufanya kazi na kubuni mbinu mbali mbali ya kujiingizia kipata,wanapoteza muda mwingi katika kushabikia wanasiasa huku wakidhani wataletewa maendeleo.yaani wanasubir wanasiasa wawaletee maendeleo.
Ni vigumu kwa mwananchi kuishi nje ya siasa kwani siasa ni " ni mfumo wa maisha wa jamii uliokubaliwa na jamii hiyo ili kujiletea maendeleo" ... hakuna mpango binafsi wa mtu utakao weza kuwa na maendeleo nje ya siasa kifupi lazima kila mtu atambue umuhimu wa kuielewa siasa ili aweze kuishiriki mijadala ya kisiasa kuleta tija ya jamii na maendeleo yake kwa ujumla.
Ushiriki wetu dhaifu ndiyo sababu tunaamuliwa mambo na wanasiasa lakini wanasiasa hawataweza kuwa miungu watu kama tukikataa kuburuzwa kwa mawazo hafifu na yasiyo na tija ya moja kwa moja kwetu.