Mkuu, ukiona mtu mzima kama kiongozi wa Taifa anapuuza ushauri wa kitaalamu basi ujue kuna agenda chafu nyuma yake. Viongozi wengi wamekuwa na tabia hiyo, na isitoshe wanaonufaika na maamuzi yao ni kundi dogo sana, natumaini tukiandika katiba mpya na kuweka vipengele ambavyo vitawabana kwa masuala kama hayo tutafanikiwa.